Unknown Unknown Author
Title:
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
HOME PICHA ZINATISHA ACHINJWA KAMA KUKU Mwili wa Mkazi wa kijiji cha Kabalenzi Kata ya Kanazi wilayani Ngara mkoan...
HOME

PICHA ZINATISHA ACHINJWA KAMA KUKU

Mwili wa Mkazi wa kijiji cha Kabalenzi Kata ya Kanazi wilayani Ngara mkoani Kagera Andrew Lazaro (36) ukiwa kitandani baada ya kuuwawa na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo Januari 28,2015 kwa kumkatakata mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake baada ya kumvamia akiwa na familia yake kijijini humo.
Kaimu Mwenyekiti wa kijiji hicho Jason Bamenya amesema kuwa marehemu alivamiwa jana saa 5 usiku  ambapo waliotekeleza mauaji hayo walimgongea mlango na kumshambulia. 
Bamenya amesema  taarifa zilizopatikana kutoka kwa mke wa marehemu ni kwamba wakati wakifungua mlango walimwangusha chini na kumshambulia kwa kumkamata na mapanga na mkewe  kumfunga kitambaa usoni.
Tumepata maelezo ya mkewe alfajiri na tulipofika tukakuta mwili wa marehemu unayo majeraha makubwa ambayo yalitokana na kucharangwa mapanga na wauaji kutokomea kusikojulikana,”- Alisema Bamenya.
Akiongea na Wanahabari,Mke wa marehemu Revina Andrew (27) amesema kuwa wakati wamelala ndani ya nyumba yao wakiwa na watoto wao wanne mumewe aliitwa na watu wakimtaka afungue mlango huku wakishikilia visu na mapanga.
Amesema aliposita kufungua walibomoa mlango huo na nyumba ikiwa imezingirwa ambapo baadhi yao waliwafunga watoto kamba na Mama huyo kumfunga kitambaa cheusi usoni kisha kumkatakata mapanga Mume wake.
Kamanda wa Polisi mkoani Kagera Henry Mwaibambe alipoulizwa kwa njia ya simu amesema Jeshi la Polisi wilayani Ngara limefika eneo la tukio lakini hajaarifiwa kukamatwa watuhumiwa wa mauaji hayo na upelelezi unaendelea.

About Author

Advertisement

Chapisha Maoni

 
Top