HOME
OME
TAZAMA PICHA- TUKIO KUBWA LILILOFANYWA NA MAASKARI POLISI WA SHINYANGA USIKU
Ufunguaji Shampeni unaendelea |
Wageni mbalimbali wakiwa eneo la tukio |
Cheeers
Meza imependeza
Kulia
ni Mgeni rasmi Annarose Nyamubi,kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga
Justus Kamugisha(katikati) na mwenyekiti wa kamati ya sherehe Pili
Misungwi kabla ya kukata keki wakati wa sherehe hizo usiku wa kuamkia
jana
Mgeni
rasmi Annarose Nyamubi akimlisha keki kamanda wa polisi mkoa wa
Shinyanga Justus Kamugisha wakati wa sherehe hizo usiku wa kuamkia jana
Askari
wawili waliaagwa wakiwa na wake zao-Kushoto ni mnadhimu 2 mkoa wa
Shinyanga Peter Nduguru anayekwenda kuwa mkuu wa polisi wilaya ya Mbulu
mkoani Manyara na mkuu wa usalama barabarani mkoa wa Shinyanga Deusderis
Rugimbana(Aliyeshikilia kipaza sauti) anayekwenda kuwa mkuu wa usalama
barabarani mkoa wa kipolisi Ilala jijini Dar es salaam.Pichani
wakijiandaa kukata keki
Sherehe inaendelea
Ukumbi ulipendeza kweli kweli
Wengine walijitokeza kucheza muziki
Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga Annarose Nyamubi akizungumza katika sherehe hiyo
ambapo aliwataka wananchi wa mkoa wa Shinyanga kuendelea kushirikiana
na jeshi la polisi katika kuimarisha ulinzi na usalama hususani katika
kipindi hiki taifa likielekea kufanya matukio makubwa mawili ya kupigia
kura katiba inayopendekezwa na uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Mkuu
huyo wa wilaya ya Shinyanga aliyekuwa mgeni rasmi kwa niaba ya mkuu wa
mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga alisema pamoja na kazi nzuri inayofanywa
na jeshi la polisi ni vyema wananchi wakashirikiana na polisi ili
kuhakikisha kuwa amani inaendelea kuwepo katika jamii.
Waandishi wa habari walikuwepo eneo la tukio
Usiku
wa kuaga mwaka 2014,kukaribisha mwaka 2015,kuaga maafisa wawili wa
jeshi la polisi Shinyanga na kupongeza maafisa 20 waliofanya kazi nzuri
mwaka 2014
Kila mmoja anajimwaga kivyakeeee
Meza zilipendeza haswaaaa
. |
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Annarose Nyamubi (wa pili kutoka kushoto) aliyekuwa mgeni rasmi akicheza muziki na wageni waalikwa mbalimbali
Burudani ilichukua nafasi yake-Picha zote na Na Kadama Malunde-Shinyanga |
Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga Annarose Nyamubi amewataka wananchi wa mkoa wa
Shinyanga kuendelea kushirikiana na jeshi la polisi katika kuimarisha
ulinzi na usalama hususani katika kipindi hiki taifa likielekea kufanya
matukio makubwa mawili ya kupigia kura katiba inayopendekezwa na
uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Nyamubi
ameyasema hayo usiku wa kuamkia jana Jumapili wakati wa sherehe ya
jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga kuaga mwaka 2014 na kukaribisha mwaka
2015 iliyokwenda sambamba na kuwaaga askari wake wawili wanaobadili
vituo vyao vya kazi na kuwapatia zawadi wafanyakazi 20 bora wa jeshi
hilo katika mwaka 2014.
Mkuu
huyo wa wilaya ya Shinyanga aliyekuwa mgeni rasmi kwa niaba ya mkuu wa
mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga alisema pamoja na kazi nzuri inayofanywa
na jeshi la polisi ni vyema wananchi wakashirikiana na polisi ili
kuhakikisha kuwa amani inaendelea kuwepo katika jamii.
“Kila
kwenye mafanikio ya polisi,nyuma yake kuna raia mwema aliyetoa
taarifa,tunaomba ushirikiano uliopo udumu hususani katika matukio ya
kitaifa yanayokuja,hakuna haja ya kuogopa polisi wananchi toeni taarifa
zitakazosaidia kuondoa uhalifu katika jamii,pia tushirikiane katika
kupiga vita ukatili wa kijinsia”,alisema Nyamubi.
Aidha
alilipongeza jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga kwa kazi nzuri na
iliyotukuka wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa 2014 kwani Shinyanga
ni miongoni mwa mikoa michache nchini ambako uchaguzi ulikamilika kwa
utulivu hapakuwa na matukio makubwa ya kutisha.
“Tumejifunza
mengi katika uchaguzi wa serikali za mitaa,sasa tunajipanga vyema kwa
ajili ya uchaguzi mkuu ujao ili uwe wa amani na utulivu,lakini yote haya
yatawezekana kama kutakuwepo ushirikiano wa wadau mbalimbali”,aliongeza
Nyamubi.
Kwa
upande wake kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha
alisema changamoto iliyopo ni upungufu wa askari polisi kwa sababu hivi
sasa askari mmoja analazimika kuhudumia wananchi 1584 wakati inatakiwa
ahudumie wananchi 350 hadi 500 hivyo ushirikiano unahitajika zaidi ili
kufanya Shinyanga kuwa mahali salama pa kuishi binadamu.
Kamanda
Kamugisha alisema nidhamu inaendelea kuporomoka kila siku hivyo
kuwataka askari wake kuendelea kuwa na nidhamu nzuri kwani nidhamu ndiyo
msingi mzuri wa kusimamia sheria.
“Mwaka
2014 haki ya nidhamu katika jeshi letu ilikuwa nzuri,japokuwa askari 7
walifukuzwa kutokana na utovu wa nidhamu na wengine 6 kubadilishwa vituo
vya kazi,hii inaonesha kiasi gani tulivyo makini na suala la nidhamu
kwani huduma yetu inagusa watu wengi,askari mmoja akionesha utovu wa
nidhamu anachafua jeshi la polisi na serikali iliyoko
madarakani”,aliongeza Kamugisha.
Katika
Sherehe hizo za kuaga mwaka 2014 na kukaribisha mwaka 2015
zilizojulikana kama “Polisi Family Day” jumla ya wafanyakazi wa polisi
mkoa wa Shinyanga walitunukiwa zawadi kwa kazi nzuri waliyoifanya katika
jeshi la polisi mwaka 2014.
Aidha
askari wawili waliagwa ambao ni afisa mnadhimu 2 mkoa wa Shinyanga
Peter Nduguru anayekwenda kuwa mkuu wa polisi wilaya ya Mbulu mkoani
Manyara na mkuu wa usalama barabarani mkoa wa Shinyanga Deusderis
Rugimbana anayekwenda kuwa mkuu wa usalama barabarani mkoa wa kipolisi
Ilala jijini Dar es salaam.
Na Kadama Malunde-Shinyanga
Chapisha Maoni