WAMILIKI WA VIWANDA WATAKIWA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADADISI WA SENSA YA VIWANDA
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Maria Bilia akizungumza
wakati wa uzinduzi wa mafunzo ya wadadisi 200 wa Sensa ya Viwanda
itayofanyika nchi nzima mwezi huu. Mafunzo hayo yanafanyika chuo cha
Takwimu Mashariki mwa Afrika kilichopo eneo la Changanyikeni jijini Dar
es salaam.
Mkuu
wa chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika kilichopo eneo la Changanyikeni
jijini Dar es salaam Prof.Ngalinda Innocent akizungumza na wadadisi
watakaokusanya takwimu za Sensa ya Viwanda mwezi huu wakati wa ufunguzi
wa mafunzo ya siku 14.
Mkuu
wa chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika Prof. Ngalinda Innocent
akizungumza jambo na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara
Bi. Maria Bilia (katikati) na Kamishna wa Sensa ya Watu na Makzi Bi.
Hajjat Amina Mrsiho Said leo jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi
Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa akizungumza na
wadadisi 200 watakaokusanya takwimu za viwanda wakati wa Sensa ya
Viwanda itakayofanyika nchini nzima mwezi huu leo eneo la Chuo cha
Takwimu cha Mashariki mwa Afrika jijini Dar es salaam.
Baadhi
ya wadadisi wa Sensa ya Viwanda wakifuatilia hafla ya ufunguzi wa
mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kukusanya takwimu sahihi wakati wa Sensa
ya Viwanda leo jijini Dar es salaam.
Kaimu
Mkurugenzi wa Shirikisho la wenye Viwanda nchini Bw.Hussein Kamote
akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya wadadisi 200 watakaokusanya
takwimu wakati wa Sensa ya viwanda itakayofanyika nchini mwezi huu.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Maria Bilia akiwa katika
picha ya pamoja na menejimenti ya NBS na wadadisi wa Sensa ya Viwanda
Picha na Aron Msigwa - MAELEZO
Na. Aron Msigwa – MAELEZO.
SERIKALI
imewataka wamiliki wa viwanda kuwapa ushirikiano wadadisi wa Sensa ya
Viwanda watakaopita katika maeneo yao kwa lengo la kukusanya takwimu
sahihi za viwanda vilivyopo nchini na mchango vinaotoa katika maendeleo
ya taifa.
Kauli
hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara
ya Viwanda na Biashara Maria Bilia wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku
14 ya wadadisi wa Sensa ya Viwanda yanayoendelea katika chuo cha
Takwimu cha Mashariki mwa Afrika kilichopo eneo la Changanyikeni jijini
Dar es salaam.
Amesema
kuwa mafanikio ya Sensa hiyo yatatokana na wamiliki wa viwanda
kuthamini na kutambua umuhimu za Sensa hiyo kwa kutoa ushirikiano kwa
wadadisi watakaopita katika maeneo yao kupata taarifa zinazohusu masuala
mbalimbali ikiwemo uzalishaji wa bidhaa na masuala ya ajira;
Amesema
upatikanaji wa takwimu sahihi kuhusu Sekta ya Viwanda nchini Tanzania
utaiwezesha Serikali kuweka Sera na mipango endelevu ya maendeleo
itakayoisaidia sekta hiyo kupiga hatua kimaendeleo.
“Sensa
hii ya viwanda ni muhimu kwa maendeleo ya nchi yetu, na mafanikio yake
yatatokana na wenye viwanda kutupa ushirikiano maana bila wao kutoa
takwimu sahihi mipango ya maendeleo kuhusu viwanda haitatekelezeka kwa
sababu ya kukosa takwimu sahihi” Amesema Bilia.
Kuhusu
sampuli ya viwanda vitakayoguswa na Sensa hiyo amesema ni pamoja na
maeneo ya viwanda yaliyoajiri watu wengi na yanayohusisha uzalishaji
mkubwa wa bidhaa za viwandani ,maeneo ya uzalishaji wa bidhaa za kokoto,
bidhaa za vyakula na maeneo yaliyoajiri mtu zaidi ya mmoja.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dkt. Albina
Chuwa akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo amesema kuwa Sensa
hiyo ya viwanda itakayohusisha viwanda vyote nchini inafanywa kwa
ushirikiano wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu na Wizara ya Viwanda na
Biashara.
Amesema
kukamilika kwa Sensa hiyo kutaliwezesha taifa kuwa na takwimu sahihi za
viwanda na kutambua mchango wa Sekta ya viwanda katika uchumi wa taifa
na mchango wa ajira kwa wananchi.
Kuhusu
mafunzo hayo ya siku 14 kwa wadadisi 200 watakaoendesha zoezi hilo
amesema Ofisi ya Taifa ya Takwimu kupitia Chuo cha Takwimu cha Mashariki
mwa Afrika inaendesha mafunzo hayo kwa vitendo na nadharia ili
kuwawezesha na kuwajengea uwezo wadadisi hao kukusanya takwimu bora.
“Lengo
la kuendesha Sensa hii ni kuhakikisha kuwa nchi yetu inapiga hatua na
kuwa nchi yenye maendeleo ya kati kwa kuwa na matumizi sahihi ya takwimu
zetu”
Kaimu
Mkurugenzi wa Shirikisho la wenye Viwanda nchini Bw.Hussein Kamote
akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo kwa niaba ya wamiliki wa
Viwanda nchini amesema kuwa Sensa ya viwanda itakayofanyika nchini mwezi
huu italiwezesha taifa kuwa na takwimu sahihi zinazohusu sekta ya
viwanda.
“Sensa
hii ya viwanda ni muhimu sana kwa maendeleo ya taifa nawaomba wenye
viwanda watoe ushirikiano wa kutosha maana bila wao zoezi hili litakuwa
gumu”
Ameongeza
kuwa Sensa ya viwanda ni muhimu kutokana na mchango wake katika nchi
nyingi za Asia ambazo zimefanikiwa na kupiga hatua kimaendeleo kwa
sababu ya kuwa Sensa endelevu na takwimu sahihi za sekta ya viwanda na
mchango wake katika pato la taifa.
HOME
Chapisha Maoni