HOME
Pamoja na kwamba ana umri wa miaka 31 lakini takwimu zake za uwanjani zinaonyesha bado ndio mchezaji aliyefiti kuliko wote kwenye ligi kuu ya Hispania na labda katika ligi zote kubwa barani ulaya. Hii inathibitishwa na dakika alizocheza msimu mpaka kufikia sasa.
Mpaka kufiki Jumapili Ronaldo ndio alikuwa mchezaji ambaye amecheza kila dakika katika mechi 34 za La Liga msimu huu.
Alitoka nje ya uwanja zikiwa zimebaki dakika mbili za nyongeza, na hivyo kuharibu rekodi yake mpya. Alicheza dakika 90 dhidi ya Getafe jumamosi iliyopita na akawa anashikilia peke yake rekodi ya kucheza kila dakika katika mechi 33 za La Liga.
Mchezaji
wa Malaga Rosales alicheza kila dakika katika mechi 32 kabla ya kukosa
mchezo wa jumamosi kutokana na kuwa na kadi, hivyo kumuacha Ronaldo kama
mchezaji pekee ambaye amecheza kila dakika ya michuano ya la liga msimu
huu.
Mpaka kufikia dakika ya 90 aliyotoka dhidi ya Villareal, Ronaldo alikuwa ameshacheza dakika 3,060 katika mechi zote 34 lakini alizoksa dakika mbili zilizoongezwa kufidia muda, hivyo kumaanisha kwamba La Liga wataweka kwenye rekodi kwamba hakumaliza mechi yote. Ligi nzima ina dakika 3,420 kwa kila mchezaji.
Ronaldo
pia amecheza dakika 899 katika Champions League, na ataweza kupata
nyingine 270 ikiwa Real Madrid watafanikiwa kufika fainali au 60 zaidi
kama mechi za nusu fainali na fainali zitaenda kwenye extra time.

Chapisha Maoni