NEWSROOM NEWSROOM Author
Title:
Author: NEWSROOM
Rating 5 of 5 Des:
HOME TABORA FERINAND Wambari, Jaji wa Mahakama Kuu, Kanda ya Tabora  ametupilia mbali hoja za mawakili wa Husna Mwilima, Mbunge wa...
HOME

TABORA


FERINAND Wambari, Jaji wa Mahakama Kuu, Kanda ya Tabora  ametupilia mbali hoja za mawakili wa Husna Mwilima, Mbunge wa Kigoma Kusini na serikali dhidi ya David Kafulila ambapo waliwasilisha nyaraka za kurasa zaidi ya 300 kuomba kesi yake (Kafulila) ifutwe.

Katika hoja zao wamesema kwamba, hawaoni kesi ya kujibu baada ya Kafulila na mashahidi wake watatu pamoja na vielelezo kupokelewa mahakamani.

Akifuta hoja hizo mahakamani Jaji Wambari amesema, Husna anapaswa kutoa ushahidi uliompa ushindi lakini pia msimamizi wa uchaguzi huo naye anatakiwa kutoa ushahidi uliosababisha amtangaze Husna kuwa mshindi.


Baada ya kauli hiyo, Jaji Wambari ameahirisha kesi hiyo na kuagiza kusikilizwa tena tarehe 3 Mei mwaka huu.

Awali, Kafulila alikuwa Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kusini ambapo mahakama iliamuru chini ya Jaji Wambari kuwasilishwa fomu halisi za Matokeo ya Uchaguzi kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Kafulila alikubali na akaiomba mahakama kuiamrisha NEC kuwasilisha fomu hizo mahakamani ili ziweze kupitiwa kwa kulinganishwa na fomu alizowasilisha mahakamani na kupelekea Kenned Fungamtama, Wakili wa Serikali kupinga ombi hilo hapo awali.


Katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25 mwaka jana, Kafulila alidai  ndiye mshindi halali wa kiti cha ubunge jimboni hapo lakini Msimamizi wa Uchaguzi alimtangaza Husna kuwa mshindi kutoka CCM badala yake.

About Author

Advertisement

Chapisha Maoni

 
Top