HOME
Bomoabomoa
iliyoanza mwishoni mwa mwaka 2015 kwenye baadhi ya maeneo jijini Dar
es salaam hasa ya mabondeni ikiwemo maeneo yaliyo kando na mto msimbazi ambapo zoezi hilo lilisitishwa baada ya kesi inayopinga ubomoaji wa nyumba takribani 2619 za wakazi wa Tabata Segerea kufunguliwa.
April 22 2016 yametolewa maamuzi ya kesi hiyo ambapo Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi
imesema kwamba kesi hiyo imekosa vigezo vya kisheria kutokana na
kutokuwa na kibali cha wananchi wote kwa pamoja kinachoruhusu watu nane
kufungua kesi badala ya wananchi wote.
Wakizungumza na millardayo.com Diwani kata ya Tabata, Patrick Assenga na wakili upande wa utetezi Abubakar Salim wamesema …..
>>>mahakama
ya juu itafsiri nini maana ya kifungu kile wanaposema ridhaa ya watu,
maombi haya yameondolewa sio kwamba yamefutwa sasa maombi yakiondolewa
tunaweza tukayaleta tena, kwahiyo tunaweza tukaenda tukaongeza hayo
maneno wanayosema hayapo tukarudisha tena au tunaweza watu wote hawa
2619 wafungue kesi moja ambayo itakuwa ni ngumu, tutajipanga tujue nini
tufanye kati ya hayo matatu:-Abubakar Salim
>>>’wamesema
kuna kasoro za kisheria zimejitokeza ambazo zimesababisha tukakosa
uhalali huo, sisi tunaenda kujipanga tutarudisha hii kesi kwa sababu
nyumba 2619 ni watu wengi sana ambapo kuna takribani ya watu elfu
arobaini na kitu hao watakosa makazi, Rais lazima aingilie kati ni suala
kubwa na limebeba maslahi ya watu wengi’:-Patrick Assenga
Chapisha Maoni