Unknown Unknown Author
Title: Mtoto Mtanzania wa miaka 16 alivyoongea kwa kujiamini mbele ya viongozi wa dunia umoja wa mataifa
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
HOME Mtoto Mtanzania mwenye umri wa miaka 16 Getrude Clement kutokea Mwanza amehutubia mbele ya viongozi mbalimbali wa dunia...
HOME
Mtoto Mtanzania mwenye umri wa miaka 16 Getrude Clement kutokea Mwanza amehutubia mbele ya viongozi mbalimbali wa dunia kwenye mkutano wa umoja wa mataifa akiwa mwenye kujiamini na kutoonekana kuwa na hofu japo anaongea kwenye jukwaa ambalo linatazamwa na viongozi mbalimbali.
Mataifa zaidi ya 150 yalitia saini makubaliano ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi ikiwemo Marekani ambapo katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki moon ndio alimkaribisha Getrude kuongea kwa kusema ‘ni furaha yangu kumualika Getrude Clement ambaye pia ni mwakilishi wa vijana anayeishi Tanzania na anaziwakilisha sauti za vijana
Getrude alianza kwa kuwasalimia waalikwa huku ikiripotiwa Maraisi 60 walihudhuria na kisha akaeleza kuwawakilisha vijana na watoto ambapo alizungumzia mabadiliko ya tabia nchi, hatari yake na kwamba wamekua wakifikisha ujumbe kwa Wananchi juu ya mabadiliko hayo kama anavyoonekana kwenye hii video hapa chini.

 VIDEO HII HAPA CHINI
Kama una habari ,picha za matukio mbalimbali nitumie WhatsApp 0719565345

About Author

Advertisement

Chapisha Maoni

 
Top