Unknown Unknown Author
Title: SERIKALI YAMILIKI KWA 100% KIWANDA CHA MATAIRI ARUSHA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
HOME DODOMA ASILIMIA 26 ya hisa zilizokuwa zinamilikiwa na mbia mwenza wa serikali, katika kiwanda cha kutengeneza matairi cha G...
HOME

DODOMA


ASILIMIA 26 ya hisa zilizokuwa zinamilikiwa na mbia mwenza wa serikali, katika kiwanda cha kutengeneza matairi cha General Tyre Arusha, zimenunuliwa na serikali na hivyo kiwanda hicho kwa sasa kinamilikiwa na serikali kwa asilimia 100.

Hayo yalibainishwa jana bungeni na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage alipokuwa akijibu swali la msingi la Mbunge wa Viti Maalumu, Catherine Magige (CCM).kiwanda“Je, ni lini serikali itafungua rasmi kiwanda cha kutengeneza matairi cha General Tyre ambacho kilikuwa mkombozi kwa uchumi wa taifa na kilichotoa ajira kwa wananchi wa Arusha?” Alihoji Magige.

Mwijage akijibu alisema serikali imeweka dhamana ya kusimamia na kuendesha kiwanda hicho, chini ya Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC) na kwamba tangazo la Serikali (GN) kuhusu uamuzi huo litatolewa wakati wowote kuanzia jana.

Alisema dhamira ya serikali ni kuona kiwanda hicho kitaanza kuzalisha matairi mapema iwezekanavyo na tayari wizara imeagiza NDC kuandaa andiko la kitaalamu, ambalo pamoja na kujibu masuala ya kiuchumi.

Pia shirika hilo litatoa majibu ya kiufundi na kijamii na kwamba ni lazima lizingatie maoni ya wadau wa sekta husika kwa ajili ya kuboresha kiwanda hicho. Aidha, mradi huo utaendeshwa chini ya menejimenti ya rasilimali watu wenye weledi katika biashara ya matairi na bila kutegemea ruzuku kutoka serikalini.

Awali kiwanda hicho kiliacha uzalishaji mwaka 2009 baada ya serikali kukosa fedha za kukiendesha huku mbia mwenza kampuni ya Continental AG, kutokuwa tayari kuendelea na uwekezaji huo.

About Author

Advertisement

Chapisha Maoni

 
Top