Wauguzi
wa zahanati ya kituo cha ustawi wa Jamii cha Bukumbi kijiji cha Kigongo
kata ya Idetemya wilayani Misungwi mkoani Mwanza wakiwaongoza waandishi
wa habari wa jiji la Mwanza na Dar es Salaam waliofika kuwatembelea
wazee wanaoishi katika kituo hicho kujua jinsi wanavyoishi na kuwa
kutambua suala la uzazi wa mpango. Ziara hiyo ya waandishi wa habari
iliyofanyika wiki iliyopita iliratibiwa na taasisi inayojishuhulisha na
ongezeko la idadi ya watu na uzazi wa mpango (TCDAA) wakishirikiana na
Marie Stopes Tanzania. Picha zote na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.
Wazee
wa kituo cha ustawi wa Jamii cha Bukumbi kijiji cha Kigongo kata ya
Idetemya wilayani Misungwi mkoani Mwanza wakiendelea na kazi za mikono.
Mmiliki wa Blog ya Kajunason akimsaidia kusuka kikapu mmoja ya wazee anayelelewa katika kituo hicho.
Moja ya nyumba wanayoishi wazee hao.
Waandishi
wa habari wa jiji la Mwanza na Dar es Salaam waliotembelea Wazee wa
kituo cha ustawi wa Jamii cha Bukumbi wakifanya mahojiano ili kujua
changamoto mbali mbali zinazowakabili ambapo wazee hao walisema jambo
kubwa linalowaumiza kicha ni upatikanaji wa matibabu katika zahanati yao
jambo linalowafanya wengine kuishi na maradhi kwa muda mrefu.
Waaandishi wakiendelea kufanya mahojiano na Wazee wa kituo cha ustawi wa Jamii cha Bukumbi.
Ofisa
Mfawizi wa Makao ya wazee wasiojiweza, Michael Bundala akifanya
mahojiano na waandishi wa habari ambapo katika mahojiano hayo alielezea
kuwa kuna changamoto nyingi za kuishi na wazee hawa kama kiongozi kwa
vile wazee wamekuwa wakorofi mno na kuona siwatendei haki katika maamuzi
ambayo nimekuwa nikiyatoa ikiwemo katika ugawaji wa vyakula.
--- Na Cathbert Kajuna - Mwanza. Wazee
wanaoishi katika kituo cha ustawi wa Jamii cha Bukumbi kijiji cha
Kigongo kata ya Idetemya wilayani Misungwi mkoani Mwanza wanaiomba
Serikali kuwapatia huduma za afya katika Zahanati ya kituo chao. Wazee
hao wanaeleza kwamba changamoto hizo katika ziara ya waandishi wa
habari wa jiji la Mwanza na Dar es Salaam waliounganishwa pamoja na
kuratibiwa na taasisi inayojishuhulisha na ongezeko la idadi ya watu na
uzazi wa mpango (TCDAA) na Marie Stopes Tanzania. Wakizungumza kwa nyakati tofauti wazee hao wanasema katika zahanati hiyo hakuna dawa na wanapoumwa wanalazimika kununua dawa. Mwenyekiti
wa kambi hiyo, Helen Emmanuel anasema wanakabiliwa na changamoto
mbalimbali za huduma ya afya pamoja na wenzao wasiojiweza kufukuzwa
kambini. "Tunapofika
katika zahanati hii daktari anatupima vizuri lakini hakuna dawa hivyo
anatuandikia kwenye karatasi anatuambia tukanunue. "Kwakweli
hii ni changamoto kubwa sana kwetu kwasababu wakati mwingine
tunapoandikiwa dawa hela ya kununulia tunakosa hali inayosababisha
tunaendelea kuumia kutokana na kwamba afya zetu ndio hizi na hatuna
sehemu ya kujipatia kipato" alisema Heleni. Pia
alisema kwa sasa wapo wazee 78 katika kambi hiyo lakini wapo walemavu
wenzao saba ambao wameambiwa wahame kambini waende vijijini wakati
hawana uwezo. "Kwakweli
inaumiza sana kwasababu hawana uwezo wa kujitafutia pia mimi sina uwezo
wa kuwasaidia kwasababu mimi mwenyewe ni mlemavu ,"alisema. Ofisa
Mfawizi wa Makao ya wazee wasiojiweza,Michael Bundala alisema hapa
kambini tuna watoto 17 ambao wazazi wao wako humu kambini na wengine
waliotimiza miaka 18 tuliwapunguza na kuwatengea eneo kwa ajili ya
makazi na tusingefanya hivyo tungekuwa zaidi ya 800 kwasababu wengine
wanapeana mimba wenyewe kwa wenyewe. Naye
Mwenyekiti wa kijiji cha Kigongo Kata ya Idetemya, Sebastian Kisumu
alisema ipo changamoto ya vijana wa nje kuwapa mimba wasichana wa kambi
hiyo. Alisema
wapo wataalamu mbalimbali mambo wanafika katika kambi hiyo kutoa elimu
ya uzazi wa mpango lakini wengi wao hawaipokei hali inayosababisha kuwa
na idadi kubwa ya watoto ambao hawana baba.
Chapisha Maoni