HOME
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amewataka wananchi wa
wanaosafiri mara kwa mara kwa ajili ya harakati zao za maisha kuchukua
vyandarua na kuvitumia wanapokuwa safarini ili kujikinga na maradhi ya
Malaria.
Akizungumza
katika Maadhimisho ya siku ya Malaria Duniani katika viwanja vya
Maisara, Mjini Zanzibar, Balozi Seif alisema licha ya Zanzibar kuwa na
kiwango cha chini ya asilimia moja cha Malaria, utafiti unaonyesha watu
wanaogunduliwa kuugua maradhi hayo hivi sasa ni wale wenye utaratibu wa
kusafiri nje ya Zanzibar.
Amesema
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imedhamiria kwa dhati kuimarisha afya
za wananchi na itaendelea kuboresha huduma za afya sehemu zote na
kuwataka wananchi kuunga mkono juhudi hizo.
Hata
hivyo alisema wakati Zanzibar inajivunia mafanikio katika vita dhidi ya
Malaria bado maradhi ya Kipindupindu yanaendelea kuwa tishio kwa
wananchi na kuwataka kufuata maelekezo yanayotolewa na wataalamu wa
afya.
Mapema
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Juma Malik Akili alisema katika kumaliza
Malaria kuanzia tarehe 25 mwezi huu watatoa vyandarua 760,000
vilivyotiwa dawa bure kwa wananchi katika Wilaya zote za Zanzibar.
Amewashauri wananchi kuvitumia vyandarua hivyo kikamilifu kwani inaonekana kuwa ndio njia kubwa inayosaidia kukinga Malaria.
Katika
maadhimisho hayo, wananchi na vikundi vya mazoezi wakiongozwa na Makamu
wa Pili wa Rais walifanya matembezi ya hiari yaliyoanza Mazizini,
Wilaya ya Magharibi B na kumalizia viwanja vya Maisara, Mjini Zanzibar.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idi (katikati) akiongoza
Matembezi ya hiari ya kuadhimisha Siku ya Malaria Duniani ambayo
yamefanyika kuanzia mazizini na kumalizikia maisara mjini Unguja.kulia
yake ni Waziri wa Afya Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo na kushoto yake ni
katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt Juma Malik Akili.
Vikundi
vya mazoezi vikiwa katika matembezi ya hiari ya kuadhimisha Siku ya
Malaria Duniani ambayo yamefanyika kuanzia Mazizini Wilaya ya Magharibi B
na kumalizikia Maisara Mjini Unguja.
Vikundi
mbalimbali vya Mazoezi vikifanya mazoezi baada ya kuwasili katika
Uwanja wa Maisara katika maadhimisho ya Siku ya malaria Duniani ambayo
yamefanyika Mjini Unguja.
Waziri
wa Afya Mahmoud Thabit Kombo (wa mwanzo ) akishiriki katika mchezo wa
kuvuta kamba kwenye maadhimisho hayo ambapo timu ya Baraza la
Wawakilishi ilipambana na Wizara ya Afya ambapo Afya ilipata ushindi.
Waziri
wa Afya Mahmoud Thabit Kombo akimkaribisha Mgeni rasmi katika
Maadhimisho ya Siku ya Malaria Duniani ambayo yamefanyika viwanja vya
Maisara Mjini Unguja.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idi akitoa hotuba ya
Maadhimisho ya siku ya Malaria Duniani ambayo yamefanyika Maisara Mjini
Unguja.kulia yake ni Waziri wa Afya Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo na
Kushoto yake ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt Juma Malik Akili.
Chapisha Maoni