Kutoka
Bungeni Dodoma Mkutano wa bunge umeendelea tena leo April 28 2016
ambapo mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe amewasilisha bungeni ripoti
mpya ya tuhuma za IPTL, Tegeta Escrow pamoja na standard Bank ya
Uingereza.
Katika mambo ambayo zitto ameyazungumzia ni
kuhusu Takukuru na kesi za ufisadi nchini ikiwemo ya Ufisadi wa
HatiFungani ya Tshs 1.2 trilioni Standard Bank ya Uingereza na Uchunguzi
wa IPTL Tegeta Escrow Account, Kuhusu hatifungani ya trilioni 1.2 ya
Standard Bank ya Uingereza Zitto amesema…….
>>>Waliopo
mahakamani ni wanaosemekena kutumika kupeleka rushwa. Mjumbe
kashtakiwa, lakini aliyemtuma hajashtakiwa na aliyepelekewa kilichotumwa
hajashtakiwa. Hapa kuna tatizo la msingi ambalo tukilitatua Serikali
yetu itaepuka masuala kama haya siku za usoni.
>>>Naomba
tupate kauli ya Serikali kuhusu jambo hili kwani ni moja ya JIPU kubwa
ambalo tunadhani Serikali inalikimbia. Serikali inaogopa nini? Serikali
inamwogopa nani? Kwanini kesi ya ufisadi wa IPTL unakaliwa kimya? Kwa
maslahi ya nani?
>>Katika
taarifa zote ambazo TAKUKURU inatoa kuhusu kesi za ufisadi, hakuna hata
siku moja wanasema kuhusu uchunguzi huu na lini wahusika waliochota
fedha za umma watafikishwa mahakamani.
Chapisha Maoni