Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter >>>@millardayo.
May 24 2016 tayari nimezikusanya na waweza kuzipitia hapa chini moja baada ya nyingine, moja ya habari kubwa ni kutoka Gazeti la Majira yenye kichwa cha Habari ‘Kitwanga atetewa jimboni, waonya, wapiga kura wataka aombwe radhi‘
Kwa mujibu wa Gazeti la Majira limesema Madiwani na wananchi hao wamedai video hiyo imechezwa kitaalamu na watu wa Teknolojia ya Mawasiliano ‘IT’ ili kufanikisha lengo la kuonesha kuwa mbunge wao alikuwa amelewa bungeni.
Hivyo wameliomba bunge lifanye uchunguzi na kubaini wale wote waliosambaza video inayoonesha Kitwanga akiwa anaongea akionekana amelewa wakati kiuhalisia hakulewa, bali alijibu maswali yote vizuri
#MWANANCHI Polisi Z'bar kumhoji Maalim Seif kuhusu masuala mbalimbali ambayo hata hivyo, hayakuwekwa wazi
#MWANANCHI Serikali yajibu upya swali lililomponza Kitwanga kutokana na maagizo ya Waziri Mkuu Majaliwa
#MWANANCHI JUVICUF imeitaka Serikali kubeba mzigo wa kushindwa kuwajibika kwa kuruhusu uingizwaji wa simu feki
#HabariLEO Wabunge wameitaka serikali kuweka mkazo ktk kuhakikisha ardhi yote nchini inapimwa
#RaiaTANZANIA Mtu mmoja Kenya apigwa risasi na kufariki baada ya polisi wa kutuliza ghasia kutumia risasi za moto
#MTANZANIA Baadhi ya wabunge wameshangazwa na kauli ya Spika kuhusu kusudio la kufunga mashine maalum kuwapima ulevi
#MWANANCHI RC Makonda, Waziri Simbachawene wahani msiba wa Kabwe, walifika kwa nyakati tofauti
ULIIKOSA VIDEO YA ALIYEKUWA WAZIRI KITWANGA AKIJIBU MASWALI BUNGENI NA KUDAIWA ALILEWA? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI
Chapisha Maoni