HOME
Akinamama
wanaoshiriki katika mradi wa kupaza sauti za wanawake wanaopambana na
mabdiliko ya tabianchi – Green Vocies katika picha ya pamoja na viongozi
wa Foundation For Women of Africa na wafadhili wa mradi huo, mara baada
ya uzinduzi wa mradi huo Madrid, Spain hivi karibuni.
Mama
Maria Tereza (katikati) - Rais wa taasisi ya Foundation for Women of
Africa akiwa na waandishi wa habari wanaotekelza mradi wa Green Voices
wakati wa hafla ya kuwakaribisha kinamama nchini Spain. Kutoka kushoto ni Secelela Balisidya, Tukuswiga Mwaisumbe, Farida Hamis, Siddy Mgumia na aliyechuchumaa Judica Losai.
Akinamama
wanaoshiriki katika mradi wa kupaza sauti za wanawake wanaopambana na
mabdiliko ya tabianchi – Green Vocies katika picha ya pamoja na uongozi
wa chuo kikuu cha Universitad Automous De Madrid, mara baada ya
kutembelea mazingira ya chuo hicho Madrid, Spain hivi karibuni.
Ziara ya mafunzo kujifunza jinsi ya kutengeneza mbolea ya mboji.
Ziara ya mafunzo kujifunza majiko yanayotumia nishati ya jua.
Ziara ya mafunzo katika chumba cha habari cha gazeti la El Pais.
Akimama na wawezeshaji wa mafunzo katika picha ya pamoja darasani.
WANAWAKE
wapatao 15 hivi karibuni walihudhuria mafunzo ya kuongeza ujuzi wa
jinsi ya kupambana na mabadiliko ya tabianchi nchini Spain. Mafunzo na
mradi huo vinafadhiliwa na Taasisi inayojihusisha na maendeleo ya
wanawake wa Afrika, ijulikanayo kama Foundation for Women of Africa inayoongozwa na Makamu wa Rais mstaafu waSpain Mama María Teresa Fernández de laVega.
Taasisi
hiyo itafanya kazi na wanawake hao 15 wa kitanzania kupitia miradi
inayosaidia nchi kupambana na mabadiliko ya tabianchi. Wanawake hao
ambao kati yao watano ni waandishi wa habari kila mmoja atatekeleza
mradi mmoja, huku waandishi wa habari wakisaidia kupaza sauti za
akinamama hao kupitia vyombo mbalimbali vya habari nchini.
Mradi huu unaojulikana kama GREEN VOICES una
lengo la kupaza sauti za akinamama kueneza ujuzi wao wa kupambana na
mabadiliko ya tabianchi ili jamii nzima ya kitanzania iweze kujifunza
zaidi na kuzitumia mbinu hizo katika kupambana na mabadiliko ya
tabianchi.
Mradi
huo unaoratibiwa hapa nchini na Mtandao wa wanahabari wa Mazingira
(EMNet) kwa niaba ya Foundation for Women of Africa unatekelezwa katika
mikoa sita ya Kigoma, Kilimanjaro, Mwanza, Morogoro, Dar es Salaam na
Pwani ukihusisha miradi ya kilimo, usindikaji, ufugaji na utafiti.
Mratibu
wa EMNet Secelela Balisidya amesema akinamama hao wanatekeleza miradi
ambayo inachangia moja kwa moja aidha kupambana au kupunguza athari za
mabadiliko ya tabianchi. Amesema miradi hiyo ni mradi wa kilimo cha miti
ya matunda mkoani Kigoma, kilimo cha viazi lishe visiwani Ukerewe
mkoani Mwanza, Ufugaji Nyuki mkoani Morogoro na Pwani na ukaushaji wa
mbogamboga kwa kutumia nishati ya jua mkoani Morogoro.
Miradi
mingine ni usindikaji wa vyakula mbalimbali kutokana na muhogo mkoani
Pwani, kilimo hai cha mbogamboga na kilimo cha uyoga mkoani Dar es
Salaam, mradi wa majiko banifu mkoani Pwani na mradi wa utafiti wa jiko
linalotumia nishati ya jua mkoani Kilimanajro.
Mradi
huo unaotarajiwa kutelekezwa kwa mwaka mmoja unatoa fursa kwa kinamama
kutoa ujuzo wao wa kupambana na mabadiliko ya tabianchi na sauti zao
kusikika. Hiyo ni kwa sabuabu kinamama wana uhusiano mkubwa na mazingira
kutokana na kazi wanazozifanya kila siku za kilimo na utunzaji wa
familia kuhusiana moja kwa moja na mazingira hivyo kuyaelewa zaidi
mazingira na jinsi ya kupambana na mabadiliko ya tabianchi.
Wakiwa
Madrid nchini Spain walikopata mafunzo wa wiki mbili katika chuo kikuu
cha Autonomus Universitad De Madrid, akinamama hao na waandishi wa
habari walijifunza kwa nadharia na vitendo jinsi nchi ya Spain
inavyokabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kuona njia ambazo na huku
nchini zinaweza kutumika kupambana na mabadiliko ya tabianchi. Mafunzo
kwa vitendo pia yalihusisha ziara za mafunzo kujifunza kilimo hai, na
jinsi nishati jua inavyoweza kusaidia kupambana na mabadiliko ya
tabianchi.
Waandishi wa habari pia walipata nafasi ya kutembelea chumba cha habari cha gazeti la Serikali ya Sapin la El Pais an kujifunza zaidi jinsi waandishi wa huko wanavyoandika habari zihusianazo na mabadiliko ya tabianchi.
Tovuti: Green Voices.
Chapisha Maoni