Unknown Unknown Author
Title: Maamuzi ya Rais wa UEFA baada ya rufaa yake ya kufungiwa miaka 6 kukataliwa kufutwa
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
HOME Rais wa shirikisho la soka barani Ulaya UEFA Michael Platini leo May 9 201...
HOME
Rais wa shirikisho la soka barani Ulaya UEFA Michael Platini leo May 9 2016 ameingia kwenye headlines, baada ya majibu ya rufaa yake ya kufungiwa miaka sita kujihusisha na soka kukataliwa kufutwa na badala yake amefanikiwa kupunguza kifungo hicho kutoka miaka sita hadi miaka minne.
Baada ya kukataliwa kufutwa kwa kifungo chake Michael Platini ametangaza kuwa atajiuzulu nafasi yake katika bodi ya uongozi wa soka barani Ulaya, Mahakama ya michezo (Court of Arbitration for Sport (Cas) ili amua kumpunguzia adhabu Jumatatu ya May 9 2016 na kumfungia kwa miaka minne.
Platini ambaye ana umri wa miaka 60 alifungiwa miaka sita kutojihusisha na soka kutokana na kukubali au kuhusika kupokea malipo ya pound milioni 1.3 mwaka 2011 kutoka kwa aliyekuwa Rais wa FIFA Sepp Blatter, malipo hayo yanatajwa kuwa hayakuwa halali na yanatajwa kuwa yalitumika kumfanyia kampeni Blatter.

About Author

Advertisement

Chapisha Maoni

 
Top