NEWSROOM NEWSROOM Author
Title: MATUKIO KWENYE KIKAO CHA 33 CHA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
Author: NEWSROOM
Rating 5 of 5 Des:
HOME  Baadhi ya mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao nchini Tanzania wakielekea ndani ya Ukumbi wa Bunge leo kusikiliza Hotuba ya M...
HOME



 Baadhi ya mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao nchini Tanzania wakielekea ndani ya Ukumbi wa Bunge leo kusikiliza Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.


Waziri wa Elimu, Sayansi na Mafunzo ya Ufundi Prof. Joyce Ndalichako akisalimiana na Mbunge wa Afrika Mashariki Mhe. Shy-Rose Bhanji nje ya Ukumbi wa Bunge leo mjini Dodoma.


Mbunge wa Mafinga Mjini Mhe. Cosato Chumi akichangia kuhusu Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki iliyowasilishwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.Augustine Mahiga leo mjini Dodoma.


Baadhi ya Mawaziri wakifuatilia michango mbalimbali ya wabunge wakati wa mjadala wa Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki iliyowasilishwa leo mjini Dodoma.


Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akizungumza jambo na Mbunge wa Iringa Mjini Mhe. Peter Msigwa nje ya Ukumbi wa Bunge leo mjini Dodoma.Wengine ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.Augustine Mahiga(kushoto) na Madiwani wa jimbo la Iringa Mjini waliolitembelea Bunge.


Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akimweleza jambo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano Mhe. Januari Makamba nje ya Ukumbi wa Bunge leo mjini Dodoma.


Wabunge kutoka mkoa wa Iringa Mhe. Augustine Mahiga, Mhe. William Lukuvi na Mhe. Peter Msigwa wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya madiwani wa Iringa mjini waliolitembelea Bunge leo mjini Dodoma.


Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Tulia Ackson akiwasikiliza waangalizi wa Uchaguzi Mkuu kutoka Umoja wa Nchi za Ulaya (EU) waliofika Ofisini kwake kuwasilisha Taarifa ya Umoja huo kuhusu Uchaguzi Mkuu uliofanyika nchini Oktoba 25, 2015.

Waangalizi wa Uchaguzi Mkuu kutoka Umoja wa Nchi za Ulaya (EU) wakizungumza na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Tulia Ackson (hayupo pichani) ofisini kwake Dodoma.
 Balozi wa Umoja wa Ulaya Mhe. Roeland Van De Geer (kulia) akimkabidhi Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Tulia Ackson Taarifa  ya kuhusu Uchaguzi Mkuu mjini Dodoma uliofanyika nchini Tanzania Oktoba 25, 2015.

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Tulia Ackson (kulia) akizungumza jambo na Waangalizi wa Uchaguzi kutoka Umoja wa Ulaya Mhe. Judith Sargentini (kushoto) na Balozi wa Umoja huo  Mhe. Roeland Van De Geer (katikati) waliofika Ofisini kwake Dodoma leo.
 Mwangalizi Mkuu wa Uchaguzi kutoka Umoja wa Ulaya Mhe. Judith Sargentini akimkabidhi Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Tulia Ackson Taarifa ya Uchaguzi ya Waangalizi wa Umoja wa Ulaya (EU) kuhusu Uchaguzi Mkuu wa Tanzania uliofanyika Oktoba 25, 2015. Hafla hiyo imefanyika leo mjini Dodoma.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Tulia Ackson (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Waangalizi wa Uchaguzi  kutoka Umoja wa Nchi za Ulaya (EU) waliomtembelea Ofisini kwake leo mjini Dodoma. PICHA/Aron Msigwa na Fatma Salum.

About Author

Advertisement

Chapisha Maoni

 
Top