HOME
Mbunge wa Dodoma Mjini na Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde leo
amefanya ziara ya kushtukiza katika kambi tiba ya GSM Foundation
inayofanywa na kikosi cha Madaktari bingwa kutoka hospitali ya MOI,
ambayo kuanzia leo imepiga kambi Dodoma baada ya kutoka katika mikoa ya
Mwanza, Singida, na Shinyanga.
Akieleza sababu za kuitembelea kambi hiyo ambayo iko katika hatua zake za mwisho kumaliza awamu ya kwanza, Mavunde amebainisha
>>>”Nimeshtushwa
na takwimu za mwaka juzi, kwamba wanaozaliwa ni 4000 na wanaorudi
hospitali kwa ajili ya tiba hawazidi 600. Hii ni hatari, ilipaswa mtu
kuchukua jukumu la haraka na nimeshukuru kusikia GSM mmefanya hilo,
hongereni sana“
Mavunde
amewataja Maafisa wa GSM na Madaktari kuwa ni watu wenye moyo wa
kizalendo ambao wanatakiwa kuigwa na jamii, wameacha familia zao na
wameamua kuokoa maisha ya watoto ambao hata hawawajui kwa sababu moja tu
kubwa na ya msingi ya utanzania.
Chapisha Maoni