Wakazi
waliojenga eneo la Iloganzila Jimbo la Kibamba Dar es salaam leo
wamebomolewa nyumba zao ambazo ni zaidi ya nyumba 400, zoezi hilo
limekuja baada ya amri iliyotolewa na Mahakama Kuu juzi.
Taarifa
zinasema eneo hilo lenye ukubwa wa heka 33, mali ya Henry Kashangaki
lilikuwa na mgogoro tangu 1997 baada ya kundi la watu 11 kuvamia na
kuanza kujenga nyumba na kuwauzia wananchi wengine.
Baada ya
eneo hilo kuvamiwa mmiliki wake aliamua kwenda mahakamani na kuwashtaki
Shaha Matibwa na wenzake kumi, kesi hiyo iliendeshwa kwa muda wa miaka
mitano na mwaka 2010 hukumu ilitolewa na Kashangaki na Matibwa
walionekana wana haki ya kumiliki hivyo walitakiwa kugawana.
Hata
hivyo, Kashangaki hakuridhika na hukumu hiyo na kukata rufaa na kwenda
Mahakama Kuu, January 2016 kesi hiyo ilitolewa hukumu na Kashangaki
alishinda, hivyo juzi Mahakama hiyo ilitoa amri nyumba zivunjwe ili
kumpisha mwenye eneo lake.
Chapisha Maoni