HOME
Bunge
la Bajeti ya Afrika mashariki kwa mwaka wa Fedha 2016/17 limeendelea
leo May 27 2016 Arusha ambapo Naibu Waziri wa mambo nje na ushirikiano
wa Afrika Mashariki, ambaye ni mwenyekiti wa Jumuiya ya Baraza la
Mawaziri, Suzan Kolimba amewasilisha bajeti ya shilingi milioni 101.1 kwa mwaka wa fedha 2016\2017.
Baada ya uwasilishaji wa bajeti hiyo Suzani Kolimba ameyazungumza haya ……….
>>>’ukisema
kwamba zinasuasua ni kutokana na kwamba uhalisia wa mambo kwa sababu
wanaleta kile walichokipata, mwaka jana bajeti ilikuwa milioni 110,
mambo yote yanafanyika kutokana na mpango wenyewe ambao sehemu kuu ni
utekelezaji wa shughuli zote zinazohusiana na Jumuiya zikiwemo zile
taasisi za jumuiya yenyewe’
>>>’Vipaumbele
ni vingi ikiwemo mambo ya Nishati, kuhakikisha kwamba tunatengeneza
system za kibenki kwa ajili ya kufanya umoja wa kifedha, hii bajeti
inakuwa inajumlisha shughuli zote zinazofanywa na Jumuiya ikiwemo bajeti
ya Mahakama, bajeti ya bunge lenyewe hili na taasisi zote zilizo chini
ya Jumuiya’:-Suzan Kolimba
Chapisha Maoni