HOME
Falme
za Kiarabu imeweka wazi mpango wake mradi mkubwa wa kujenga mlima lengo
ikiwa ni kuongeza mvua, taifa hilo ambalo ni jangwa lina matumaini ya
mradi huo mkubwa kuwa utasaidia kutengeneza mawingu ambayo yataleta
mvua.
Wanasayansi
kutoka Kituo cha Taifa cha Utafiti wa Anga ( NCAR ) kinachoendeshwa na
US-based University Corporation for Atmospheric Research (UCAR) kwa
sasa wako katika awamu ya kwanza ya utafiti wa kina ili kuamua juu ya maeneo ya kujenga mlima huo na urefu na upana utakaohitajika.
Mtaalam wa mipango ya hali ya hewa ya muundo kutoka (NCAR), Roelof Bruintjes aliiambia Arabian Business kuwa………>>> “Kujenga mlima si jambo rahisi, bado tunamalizia kufanya mlinganisho wa maeneo hasa tukiangalia hali ya hewa”
>>>”Kama
mradi utaonekana kuwa na gharama kubwa mno kwa serikali, mradi unaweza
usiendelee lakini hii itawapa wazo au njia mbadala ya muda mrefu kwa
ajili ya baadaye na Kama mradi utaendelea mpaka awamu ya pili tutakwenda kwenye kampuni ya uhandisi kuamua kama inawezekana au la“
Source: http://www.independent.co.uk/news/world/middle-east/uae-build-mountain-fake-increase-rainfall-rain-man-made-cloud-seeding-a7013461.html
Chapisha Maoni