Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter>>>@mathewmalunde Zote nakusogezea hapa chini.
Moja ya stori kubwa May 29 2016 ni hii kutoka gazeti la Nipashe yenye kichwa cha habari ‘Sakata la vyeti feki lawa gumzo kwa wabunge’. Gazeti hilo limeripoti kuwa siku moja baada ya serikali kutangaza kuwa itachunguza uhalali wa vyeti vya watumishi wa umma wakiwamo wabunge, uongozi wa Bunge umesema hauna kipingamizi kuhusu uamuzi huo.
Katika mahojiano na Nipashe Naibu Spika wa Bunge, Tulia Akson alisema uongozi wa Bunge hauna kipingamizi juu ya kukagua vyeti vya elimu vya wabunge ingawa bado haujapewa barua rasmi kuhusu uamuuzi huo.
#MWANANCHI Maalim Seif atikisa Z'bar aanza ziara siku sita, mabomu yarindima kutawanya wafuasi, baadhi wajeruhiwa
#TanzaniaDAIMA Serikali yaisimamisha Sahara Energy kufuatia kuingiza mafuta ya ndege yaliyochanganywa na petroli
#MTANZANIA Baadhi ya wafanyabiashara wadai wenzao wanatoa rushwa bandarini na kusababisha ukiukwaji wa utaratibu
#MWANANCHI Taasisi ya Utafiti Repoa imesema 47% ya walimu hutoroka kufundisha hivyo kutishia mustakabali wa elimu
Chapisha Maoni