NEWSROOM NEWSROOM Author
Title: Tamko la ACT Wazalendo baada ya wabunge wa upinzani kufungiwa
Author: NEWSROOM
Rating 5 of 5 Des:
HOME By Baada ya Kamati ya Maadili, Haki na Madaraka ya Bunge kuwatia hatiani wabunge saba kwa makosa mbalimbali ikiwemo kud...
HOME
By
Baada ya Kamati ya Maadili, Haki na Madaraka ya Bunge kuwatia hatiani wabunge saba kwa makosa mbalimbali ikiwemo kudharau madaraka ya bunge ambapo wabungeEasther Bulaya na Tundu Lissu wameadhibiwa kutokuhudhuria vikao vilivyobaki vya mkutano wa tatu na vikao vyote vya mkutano  wa nne.
Wabunge Pauline GekuHalima MdeeZitto Kabwe, Godbless Lema wamepewa adhabu ya kutokuhudhuria vikao vyote vilivyobaki vya mkutano wa tatu na Mbunge John Heche hatohudhuria vikao kumi vya mkutano wa tatu. Makosa hayo waliyafanya mkutano wa pili mwezi January.
Baada ya adhabu hiyo kwa wabunge, ACT Wazalendo wametoa tamko lao ambapo wameyazungumza haya………>>>’Chama cha  ACT Wazalendo kimesikitishwa na kitendo cha ugandamizaji wa demokrasia kilichofanywa na wabunge wa CCM kwa kuwasimamisha ubunge wabunge wa upinzani akiwemo kiongozi wa chama chetu  Zitto Kabwe’
>>>’Katikati ya masikitiko hayo tunafarijika kuona wabunge hao wameondolewa kwa sababu ya misimamo yao ya kutetea maslahi ya wananchi’
>>>’Tungesikitishwa zaidi kama mashujaa wetu hawa wangeondolewa bungeni kwa sababu ya ulevi au wawe sehemu ya wagonga mihuri ya masuala ya hovyo hovyo yanayosimamiwa na serikali ya chama cha Mapinduzi (CCM)’
>>>’Kwa sababu hiyo ya kusimamia maslahi ya wananchi sisi kwetu ni mashujaa na kwa maana hiyo Chama chetu kinaandaa maandamano makubwa jijini Dar Es Salaam kuwapokea mashujaa wa wananchi’
ULIKOSA HII YA ESTER BULAYA “KUNA WATOTO WENGINE BILA KUCHUKULIWA NA WABUNGE WANGEFANYIWA VITU VYA AJABU”.


About Author

Advertisement

Chapisha Maoni

 
Top