Mei 11 2016 Bunge la 11 limeendelea Dodoma, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imewasilisha hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya fedha kwa mwaka 2016/2017
Nakukutanisha na Mbunge wa Sengerema William Ngeleja lipokuwa akichangia maoni yake….
>>>‘Ninaombi
langu la muda mrefu, Wilaya ya Sengerema tuna hospitali teule ambayo
inamilikiwa na watu binafsi. Leo hii hospitali ile inaweza kutoa huduma
kwa wagonjwa kwa kuzingatia uwezo wa sasa wa vitanda 375’
‘Naomba
kupatiwa ufafanuzi wa ruzuka katika hospitali ya Sengerema, eneo hili
la huduma ya afya ni muhimu sana, tuangalie namna tunavyoweza
kurekebisha bajeti zetu tukawezesha bohari za madawa kuwafikia wananchi
wetu katika kufungua maduka ya madawa katika Wilaya zetu’
‘Ombi
langu ni ujenzi wa hospitali zinazomilikiwa na Serikali yenye hadhi ya
Rufaa katika kanda ya ziwa, pamoja na kuwa na hospitali ya Bugando
kwakweli imezidiwa. Hii ndio kanda yenye mikoa mingi zaidi lakini ina
hospitali mojatu ya rufaa’
‘Hizi huduma za wazee linahitaji ufuatiliaji ufuatiliaji wa makini, naomba sana wazee wetu hawa tuwazingatie sana ’
Unaweza kuendelea kumsikiliza kwenye hii video hapa chini…
ULIIKOSA HII WIZARA YA AFYA IMEWASILISHA BAJETI YAKE YA BILIONI 845?
Chapisha Maoni