HOME
Na Mwandishi wetu Washington
Wazanzibari waishio nchi za nje wametakiwa kuwekeza nyumbani kwa ajili ya kusaidia maendeleo ya taifa.
Wito
huo ulitolewa jana na maofisa kutoka Benki ya watu wa Zanzibar (PBZ) na
Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zaznzibar (ZSSF) wakati wakizungumza na
Wazanzibari waishio nchini Marekani.
Akizungumza
kwenye mkutano huo uliondaliwa na Jumuiya ya Wazanzibari waishio nchini
Marekani (ZADIA), Meneja wa Mipango na Uwekezaji kutoka ZSSF Bwana
Khalifa Muumin Hilal alisema kuwa Taasisi yake ina miradi kadhaa ya
uwekezaji inayoendeshwa kwa ushirikiano na Benki ya Watu wa Zanzibar, na
kwamba inawahamasisha Wazanzibari waishio Ughaibuni kuwekeza katika
miradi hiyo.
Miongoni
mwa miradi hiyo ni mradi wa nyumba za kisasa katika eneo la Mbweni, nje
kidogo ya Mji wa Zanzibar ambao ujenzi wake tayari umeanza na
unatarajiwa kukamilika katika kipindi cha miaka mitatu.
Bwana
Hilal alifafanua kuwa eneo hilo litakuwa na majengo ya nyumba za kuishi
yenye urefu wa ghorofa saba, ambapo kila ghorofa itakuwa na nyumba
mbili.
"Kutakuwa
na nyumba za vyumba viwili, vitatu na vinne" alifafanua Meneja Hilal,
na kuongeza kuwa nyumba hizo zitapatikana kwa bei nafuu.
Akijibu
swali kukhusu masharti ya upatikanaji wa nyumba hizo, Bwana Hilala
alifafanua utaratibu wa upatikanaji wake kwa kusema "Kwanza kabisa
tunaangalia vigezo vya fedha, kwa maana ya kipato cha mtu, kuna fomu ya
maombi unajaza, kisha tunakupatia fomu ya mkataba ambayo inaelezea
masharti yote, na tunaendelea kutoka hapo".
Aliendelea
kusema kuwa nyumba hizo zitapatikana kwa njia za mkopo au fedha taslim,
ambapo ukilipa fedha taslim utapata punguzo lisilozidi asiliam tano
(5%).
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Tawi la Muamala wa Kiislamu katika Benki ya
Watu wa Zanzibar Bwana Said Muhammed Said, alisema "Tumeweka utaratibu
ili kila mtu aweze kumudu kununua nyumba hizo, na hapo ndipo inapokuja
nafasi ya Benki".
Aliendelea
kusema kuwa, baada ya kujaza mikataba na ZSSF, mwekezaji ambaye hana
uwezo wa kulipa fedha taslim anaweza kwenda kwenye Benki yake na kupata
mkopo wenye masharti nafuu.
Akijibu
swali kukhusu iwapo mtu atafariki kabla ya kumaliza kuilipia nyumba
hiyo, Bwana Said alitoa khofu kwa kusema "Mtu haki yake haipotei".
Aliendelea kuwa mtu akifariki kuna hali mbili, ama nyumba itauzwa na
haki ya marehemu kupewa warithi wake, au warithi wakiamua kuendelea
kulipa basi wataendelea kubaki na nyumba yao.
Kukhusu
taratibu za malipo, Bwana Hilal alisema, mtu anaweza kulipa kila mwezi,
miezi mitatu au kama atakavyojaza kwenye mkataba wa mauzo.
Mbali
na nyumba za kuishi, eneo hilo pia litajumuisha viwanja vya watoto,
michezoya aina mbalimbali, mabwawa ya kuogelea, kituo cha Mikutano
Msikiti na mengineyo.
Akijibu
swali iwapo mikopo ya nyumba hizo itakuwa na riba au la, Bwana Said
alisema "Unachagua, kama unataka mkopo wenye riba au mkopo kwa kupitia
tawi letu la Muamala wa Kiislamu, huo utakuwa hauna riba".
Alendelea
kufafanua kuwa kiwango cha riba rubuni vinategemea na hali ya soko kwa
wakati ule mteja atakapochukua mkopo ikiwemo thamani ya sarafu kwa
wakati ule, viwango vya riba vinavyowekwa na Benki Kuu ya Tanzania na
urefu wa muda wa mkopo wenyewe.
Kukhusiana
na khofu ya mtu kupoteza nyumba yake iwapo atapoteza kazi, Bwana Said
aliwatoa khofu Wazanzibari kwa kusema "Kutolipa mkopo kwa wakati
uliokubaliwa kulaleta athari katika mfumo wa Benki.
Hata
hivyo, iwapo mtu atashindwa kulipa kwa mara ya mwanzo na ya pili
tunamtumia barua ya ukumbusho. Mara ya tatu ikiwezekana tunakutana naye
ana kwa ana na kutafuta ufumbuzi" Ama iwapo mtu atapoteza kazi milele
kwa sababu zisizoweza kuepukika kama ugonjwa na mengineyo, Mkurugenzi
huyo alisema "Tutazungumza naye ili kuiuza nyumba na kumrejeshea chake".
"Tutakuwa na mkataba maalum, na yote hayo tuliyoyazungumza yatakuwemo humo", alisisitiza Bwana Said.
Mradi
wa Makaazi ya Mbweni ni hatua za awali zilizopangwa kutekelezwa na
ZSSF, kwani baadaye kutakuwa na mpango wa ujenzi wa nyumba moja moja
(bungalow).
Hata
hivyo, Mkurugenzi Said alisema kuwa mtu akiwa na kiwanja chake binafsi,
basi pia PBZ inaweza kutoa huduma za kifedha kugharamia ujenzi wa
nyumba binafsi. "Muhimu uwe na hati miliki ya kiwanja, uwe na mkandarasi
anaye julikana, na siyo mafundi wa vichochoroni", alifafanua Bwana
Said.
Akijibu
hoja juu ya sheria inayowazuia raia wa kigeni kumiliki ardhi Zanzibar,
Meneja Hilal alifafanua kwa kusema "Ardhi ni milki ya Serikali, lakini
serikali inaruhusu ukodishaji wa ardhi kwa wawekezaji. Hata sisi ZSSF
tumekodishwa tu ardhi hiyo ya Mbweni, lakini kuna sheria ya umiliki wa
nyumba kwenye majengo ya ghorofa, na sheria hii haimbagui mtu yeyote".
Aliongeza
kuwa kila mtu atapewa hati ya umiliki wa nyumba katika ghorofa hizo
bila kujali uraia wake. "Ndiyo maana tumekuja kwenu" alisistiza Bwana
Hilal.
Baadhi
ya wachangiaji kwenye mkutano huo waliezea wasiwasi wao kuwa nyumba
hizo huenda zikatolewa kwa upendeleo kama ilivyotokea kwenye nyumba za
eneo linalojuilikana kama "Kwa Mchina". Awali nyumba hizo zilikusudiwa
kuwasaidia watu wenye vipato vya chini, lakini badala yake zikatolewa
kwa upendeleo na kumalizikia mikononi mwa watoto wa Wakubwa. "Je kuna
uhakika gani kuwa mradi wa nyumba za Mbweni hautomalizikia kuwa kama ule
wa Kwa Mchina"? aliuliza mchangiaji mmoja.
Akijibu
hoja hiyo, Bwana Hilal alisema kuwa, hilo halitotokea. Zitatolewa kwa
usawa kwa mtu yoyote yule mwenye uwezo, na ndiyo maana tumekuja Marekani
kuunadi mradi huu, ili kila mtu mwenye uwezo akiwa Mzanzibari au laa,
ndani au nje ya nchi aweze kununua nyumba hizo.
Maofisa
hao wa kutoka Benki ya Watu wa Zanzibar na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii
Zanzibar wapo nchini Marekani kuhudhuria Kongamano la Wanadiaspora wa
Tanzania (DICOTA) lilloifanyika katika Jimbo la Texas.
Bwana
Hilal alielezea shukurani zake kupata fursa ya kuzungumza na
Wazanzibari nchini hapa, na kuelezea matmaini yake kuwa mkutano huo
hautokuwa wa mwisho bali wa mwanzo kwa jili ya kuendeleza maslahi ya
Zanzibar.
Kwa maelezo zaidi juu ya mradi huo tembelea http://zssf.org/en/, na fomu za maombi zitapatikana hapo katika wakati mwafaka.
Chapisha Maoni