HOME
Msimamizi
wa Mradi wa Mabadiliko ya Tabia Nchi Wizara ya Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Geofrey Mchau akitoa mada mbele ya
Waandishi wa Habari kuhusu mabadiliko ya tabianchi nchini wakati wa
Semina Maalum kwa Waandishi hao leo 3 Mei, 2016 Jijini Dar es Salaam.
Afisa
Habari toka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Bwana Saidi Makola
akichangia mada mbele ya Waandishi wa Habari kuhusu mabadiliko ya
tabianchi nchini wakati wa Semina Maalum kwa Waandishi hao leo 3 Mei,
2016 Jijini Dar es Salaam.
Dkt.
Azma Simba wa Kitengo cha Epidemolojia Wizara ya Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ambaye alimwakilisha mgeni rasmi katika
ufunguzi wa Semina kwa Waandishi wa Habari kuhusu mabadiliko ya
tabianchi akisoma taarifa ya Mkurugenzi toka Wizarani leo 3 Mei, 2016
Jijini Dar es Salaam.
Afisa
Habari toka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Bi. Catherine Sungura akichangia mada mbele ya Waandishi wa Habari
kuhusu mabadiliko ya tabianchi nchini wakati wa Semina Maalum kwa
Waandishi hao leo 3 Mei, 2016 Jijini Dar es Salaam.
Na Benedict Liwenga-MAELEZO.
Wanahabari
nchini wametakiwa kushirikiana na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto katika kuelimisha na kuhamasisha jamii kuhusiana
na mabadiliko ya hali ya hewa na afya.
Akiongea
kwa niaba ya Mkurugenzi wa Huduma za Kinga Bi. Neema Rusibamayila wa
Wizara hiyo, Dkt. Azma Simba wa Kitengo cha Epidemolojia amesema kuwa
suala la kuielimisha jamii lina umuhimu ndo maana kuna haja ya Wizara
kushirikiana kwa pamoja katika kutekeleza suala hilo.
Ameeleza
kuwa Shughuli za kibinadamu zinachangia kwa kiasi cha asilimia 95
katika kuzalisha na kuongeza kiasi cha gesi joto katika kwenye anga hewa
ambapo amezitaja baadhi ya shughuli hizo zikiwemo za uzalishaji
viwandani, uzalishaji nishati, kilimo,ufugaji, ukataji miti, uchomaji
misitu, usafirishaji, pamoja taka.
Akitaja
athari za mabadiliko ya tabianchi, Dkt. Azma ameeleza kuwa ni pamoja na
kuongezeka kwa joto juu ya wastani, ukame, mafuriko, vimbunga,
kubadilika kwa mgawanyo na muda mvua kunyesha pamoja na kuongezeka kwa
kina cha bahari.
‘’Sisi
sote ni mashahidi wa mabadiliko ya hali hewa yalivyokuwa tishio katika
afya ya binadamu. Mabadiliko hayo yameendelea kuleta athari mbalimbali
kwa jamii, mazingira na afya ikiwemo upatikanaji wa maji safi na salama,
hewa safi, uhakika wa upatikanaji wa chakula na makazi salama’’,
alisema Dkt. Azma.
Ameongeza
kuwa athari hizo zimepeleke uwepo wa magonjwa ya kuambukiza na yasiyo
ya kuambikiza ikiwemo malaria, kuhara, kipindupindu, homa ya bonde la
Ufa, denge, utapiamlo, magonjwa ya mfumo wa upumaji na magonjwa ya mfumo
wa fahamu.
‘’Jamii
ina fursa ya kuboresha afya yake na vizazi vijavyo endapo itaamua
kubadilisha mfumo wa maisha unaochangia uzalishaji na ongezeko wa
jotogesi unaoharibu (ozone) yaani tabaka hewa’’, aliongeza Dkt. Azma.
Kwa
upande wake Msimamizi wa Mradi wa Global Framework For Climate Services
toka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Geofrey Mchau amesema kuwa halli ya hewa na tabianchi vinaweza
kubadilika kiuhalisia (Naturally) au binadamu wenyewe ambapo amefafanua
kuwa lengo la semina hiyo ni kuoingeza wigo wa matumizi wa taarifa ya
hali ya hewa katika sekta mbalimbali ikiwemo afya pamoja kuwajengea
uwezo Wataalam katika ngazi ya Wizara kimkoa pamoja na Wilaya.
‘’Tupatapo
taarifa zinazohusiana na masuala ya hali ya hewa toka Mamlaka ya Hali
ya Hewa tunazitafsiri na tunazitumia kwa manufaa ya jamii’’, alisema
Dkt. Mchau.
Naye
Afisa Habari toka Hospitali ya Taifa Muhimbili Bwana Saidi Makola
ameeleza kuwa tafiti zinazoendelea zinaonyesha kuwa kuna ongezeko la
magonjwa yatonayo na mfumo wa hewa na hayo yanatokana na mabailiko ya
tabianchi, hivyo uwepo wa semina hiyo kwa Wanahabari utasaadia kutambua
masuala mbalimbali na kuwajengea uwezo katika kuelimisha jamii.
Aidha,
Afisa Habari toka Wizarani hapo, Bi. Catherine Sungura amewaasa
Wanahabari kuzingatia katika kutafuta taarifa mbalimbali ili kuweza
kuelimisha jamii kuhusiana na masuala mbalimbali yanayohusu afya.
Semina
hiyo imehusisha Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto ikiwemo Ofisi ya Makamu wa Rais, Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA).
Chapisha Maoni