Mwenyekiti
wa mamlaka ya mji mdogo wa Chalinze Hussein Mramba akizungumza na
wafanyabiashara mbali mbali wa kitongoji cha Pera Chalinze katika
mkutano ulioandaliwa kwa ajili ya kujadili namna ya kupambana na mlipuko
wa ugonjwa kipindu pindu.
KATIKA
kuunga mkono juhudi za serikali katika kupambana na magonjwa ya
mlipuko ikiwemo kipindupindu wafanyabiashara mbali mbali katika
kitongoji cha Pera halmashauri ya Chalinze Mkoa wa Pwani wameungana na
kuanzisha kampeni maalumu kwa ajili ya kutokomeza taka zote zinakuwa
zikitupwa ovyo.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti katika kikao kilichoandaliwa kwa ajili ya kuweza
kujadili mambo mbali mbali kuhusiana na suala la usafi pamoja na
kupanga mikakati ya kuweza kuhakikisha wanapambana vilivyo na mlipuko
wa ugonjwa wa kipindu pindu.
Wafanyabishara
hao akiwemo Rashid Kirumbi,William Mshauri Pamoja na Mwanaidi
Tambiligogo walisema kwamba kwa sasa wanafanya kazi zao katika wakati
mgumu sana kutokana na kitongoji hicho cha pera hakina eneo la kutupia
taka hivyo kusababisha kuzagaa kwa uchafu mwingi ambao unaweza kuleta
madhara makubwa kwa wananchi wa eneo hilo.
Aidha
walisema kwamba kwa sasa katika eneo hilo la pera hakuna eneo maalumu
kwa ajili ya kutupia taka ukizingatia na wafanyabiashara hao wanazalisha
taka nyingi kwa siku hivyo hivyo kuwapa wakati mgumu pindi wanapotaka
kutupa taka.
“Hapa
kitu kikubwa kikao hiki kimeandaliwa kwa lengo a kuweka mikakati ya
kupambana na mlipuko wa magonjwa hususan ugonjwa wa kipindupindu ambao
kwa sasa umeongia katika eneo hili kwa hiyo sisis kama wafanyabiashara
inatubidi tuhakikishe kwamba tunafanya usafi katika maeneo yetu ambayo
tunafanyia biashara na hili suala inabidi wote kwa pamoja tushirikiane
na serikai yetu,”walisema wafanyabiashara hao.
Pia
walibainisha kuwa kwa sasa wanajipanga kwa ajili ya kuhakikisha kuwa
wanatafuta eneo maalumu la kutupia taka hizo, pamoja na kuwa na gari
ambalo litakuwa likipita katika maeneo mabali mbali kwa ajili ya kuweza
kuzikusanya taka hizo la kwenda kuzipeleka dampo.
Nao
wajumbe wa serikali ya kitongoji hicho cha pera akiwemo Simon Mbena
pamoja na Nadhil Abdallah walisema kwamba kwa sasa hali ya ugonjwa wa
kipindu pindu katika eneo hilo ni mbaya hivyo kunahitajika juhudi za
makusudi katika kufanya usafi katika sehemu za biashara na majumbani
ikiwemo sambamba na kutenga eneo kwa ajili ya dampo maalumu la
kutupitia taka hizo.
Awali
akifungua kikao hicho Mwenyekiti wa mamlaka ya mji mdogo wa Chalinze
Hussein Mramba amekiri kutokuwepo kwa eneo la serikali lililotengwa
katika kitongoji hicho kwa ajili ya matumizi ya kutupa taka,na
kubainisha kwamba tayari kuna wagonjwa watano wa kipindu pindu ambao
tayari wamesharipotiwa hivi karibuni katika eneo la Chalinze.
Mramba
alisema kwamba nia ya serikali ni kuweza kuhakikisha kwamba wanapambana
na ugonjwa huo wa kipindu pindu hivyo atashirikiana bega kwa began a
wananchi wa kitongoji hicho cha pera ili kuweza kulitafutia ufumbuzi
suala hilo na kuongeza kuwa kwa sasa wapo katika hatua za awali za
kutafuta eneo maalumu kwa ajili ya kutupia taka.
KITONGOJI
hicho cha Pera kilichopo katika mamlaka ya mji mdogo Chalinze Wilaya ya
Bagamoyo Mkoa wa Pwani hakina dampo la kutupia taka, na kupelekea
wafanyabiashara na wananchi kuamua kuzitupa sehemu yoyote hali ambayo
inachangia kwa kiasi kikubwa kuzagaa kwa uchafu huo ambao umedai
unasababisha kutokea kwa magonjwa ya mlipuko hasa katika kipindi hiki
cha masika.
Chapisha Maoni