Unknown Unknown Author
Title: ZANZIBAR YASHEREHEKEA SIKU YA WAUGUZI DUNIANI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
HOME Brasbendi ya Chipkizi ikiongoza matembezi ya wauguzi yakipita katika maeneo ya Kisonge kuelekea Studio za Rahaleo ambapo sh...
HOME
Brasbendi ya Chipkizi ikiongoza matembezi ya wauguzi yakipita katika maeneo ya Kisonge kuelekea Studio za Rahaleo ambapo sherehe hizo ziliadhimishwa rasmi.
Waandamanaji wakiingia kwa furaha eneo la Studio za Rahaleo ambapo sherehe za sikuya Waguzi Duniani ziliadhimishwa.
Mrajis Baraza la Wauguzi na Wakunga Zanzibar Vuai Kombo Haji akiongoza kiapo cha wauguzi katika maadhimisho ya siku ya wauguzi Duniani yaliyofanyika Ukumbi wa Sanaa Rahaeo.
Mkurugenzi Tiba Katika Wizara ya Afya Dkt. Salhia Ali Muhsin akimkaribisha mgeni rasmi Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo aliemwakilishi Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein katika maadhimisho hayo.
Baadhi ya wauguzi walioshiriki maadhimisho hayo wakifuatilia hotuba zilizokuwa zikitolewa katika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo, Mjini Zanzibar.
Waziri wa Afya Mhmoud Thabit Kombo aliemuwakilisha Mke wa Rais wa Zanzibar akisoma hotuba katika maadhimisho ya siku ya wauguzi Duniani yaliyofanyika Ukumbi wa Sanaa Rahale Mjini Zanzibar.
Picha ya pamoja ya baadhi ya viongozi wa wauguzi na Mgeni rasmi, Waziri wa Afya Mhmoud Thabit Kombo. Picha na Makame Mshenga Maelezo Zanzibar.

Muhimbili Kutoa Tiba Wagonjwa wa Homa Sugu ya Ini.

 Mtaalamu kutoka Marekani, Dk Brian McMahon akizungumza na madaktari na wauguzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) kuhusu tiba ya homa sugu ya ini inayosababishwa na virusi vya Hepatitis B. 
  Dk Aaron Haris kutoka Marekani akielezea jinsi mradi huo utakavyowanufaisha Watanzania ambao wameambukizwa virusi vya vya Hepatitis B. 
Madaktari na wauguzi wakimsikiliza Dk McMahon wakati akielezea kuanza kwa mradi wa tiba ya homa ya ini kwa watu mbalimbali. 
 Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Tumbo, Dk John Rwegasha (kushoto) akifuatilia mada iliyowasilishwa na Dk Edwin Masue na Dk Eva Uiso wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Wengine ni Dk McMahon na Dk Haris kutoka Marekani.
Dk Edwin Masue wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) akiwasilisha mada kuhusu dalili za homa sugu ya ini inayosababishwa na virusi vya Hepatitis B.
Picha zote na John Stephen, Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).

Na Neema Mwangomo-MNH.
Hospitali ya Taifa Muhimbili-MNH-inatarajia kuanza kampeni ya kupima na kutoa tiba kwa  ugonjwa wa Homa Sugu ya Ini ambao  unasababishwa  na Virusi vya  HEPATITIS B .
 
Daktari Bingwa wa magonjwa ya Mfumo wa Chakula na Ini  katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Edwin  Masue amesema kundi la ndio limeonekana kuathirika zaidi  kwa kuwa mtoto anapata maambukizi kutoka kwa mzazi  .
 
Kwa mujibu wa Dk. Masue mtoto anapozaliwa lazima apatae chanjo,  na pia mama mjamzito ambaye anagundulika kuwa ana Virusi vya HEPATITIS B  hupatiwa dawa ya  kumkinga mtoto katika miezi mitatu ya mwisho kabla ya kujifungua .
“Tuangalie uwezekano ili watu waelewe tatizo hili mapema , wapime na wawahi kupata matibabu kwani maambukizi makubwa yanatoka kwa mama kwenda mtoto  na kwa wale wanaoanza kutumia dawa za VVU wanatakiwa kupima ugonjwa wa homa ya Ini kwa kuwa virusi vinaingiliana,”  amesema Dk . Masue .

Mkakati wa MHN.
Kwa upande wake Daktari John Rwegasha amesema katika kipindi cha Julai mwaka huu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili  kutaanzishwa mradi wa miaka mitano ambao unalenga kupima na kutibu watu ambao watagundulika kuwa na homa sugu ya ini  na kwamba hata baada ya kukamilika kwa mradi huo wananchi wataendelea kupatiwa matibabu bure.

 “ Kuna muongozo wa tiba wa  Shirika la Afya Duniani-WHO- ambao umetolewa mwaka jana hivyo tunataka kuangalia matumizi ya huo muongozo kwenye nchi zetu za Dunia ya tatu , kuna watu wametusaidia tulikuwa hatuna uwezo wa dawa. Awali tulikuwa tunaazima dawa kwenye mradi wa HIV hivyo kupitia mradi huo tutakuwa na dawa pamoja na vitenganishi vya kimaabara,” amesema Dk Rwegasha.

“Kati  ya watu 100, wanane wanatembea na ugonjwa huo bila kufahamu baada ya miaka 20 mtu anapata matatizo ya ini na kusababisha ini kushindwa kufanya kazi na  tumbo kuvimba   hivyo natumia fursa hii kuwaambia wananchi wajitokeze kupima mapema ili waweze kupatiwa  matibabu,” amesema.

Virusi vinavyoenea:
Kwa mujibu wa watalaam , asilimia kubwa ya Virusi vya HEPATITIS B vipo kwenye damu , mbegu za kiume  , ute wa mwanamke na hedhi ya mwanamke  na kwamba  maambukizi yake hayana tofauti na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi.
Dalili za ugonjwa huo:
-Kichefuchefu
-Kukosa hamu ya kula
-Macho kua ya njano
-Mkojo kuwa wa njano
-Kupata choo chenye rangi ya njano ambayo imepauka
-Mwili mzima kuishiwa nguvu.
Hata hivyo dalili hizo si zote zinaenda pamoja , kuna wengine huwa hawana dalili hizo  kabisa.

About Author

Advertisement

Chapisha Maoni

 
Top