SHINYANGA
Kumetokea tukio la aina yake leo katika manispaa ya Shinyanga ambapo vipande vya miili ya binadamu waliozikwa katika makaburi ya watu wasiokuwa na ndugu vimeokotwa mtaanimajira ya saa moja asubuhi na kuwaacha midomo wazi wakazi wa eneo hilo.
Malunde1 blog huwa haipitwi na matukio,mwandishi mkuu wa mtandao huu ,Kadama Malunde amefika katika eneo la tukio na kujionea hali halisi ilivyokuwa makaburini.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo wamesema vipande vya miili ya binadamu vimeokotwa katika mtaa wa Butengwa kata ya Ndembezi baada ya makaburi ya watu wasiokuwa na ndugu yaliyopo katika mtaa wa Mageuzi kata ya Ngokolo katika manispaa ya Shinyanga kufukuliwa na fisi.
Inaelezwa kuwa vipande vingine vya miili mingine ya binadamu ikiwemo mifupa vimekutwa katika makaburi hayo huku makaburi mawili yakiwa yamefukuliwa na miili ya binadamu ikiwa imefunikwa na mifuko ya sandarusi.
Akizungumza na Malunde1 blog mjumbe wa serikali ya mtaa wa Butengwa Peter Joseph ambako vipande vya miili ya binadamu vimeokotwa anasimulia…
“Asubuhi nimepewa taarifa kuwa kuna vipande vya nyama karibu na nyumba ya Mama Milika wakidai pengine ni vya binadamu..nilifika eneo hilo nikajionea kipande kikubwa cha nyama ambacho mwanzo tulidhani ni mfupa wa mguu wa ng’ombe maarufu kongolo”,anasema Joseph.
“Kile kipande kilikuwa kimeliwa vidole havikuonekana…utokana na utata wa tukio hilo nikawapigia simu viongozi wenzangu wa mtaa na wa mtaa wa jirani na pia polisi,tukaenda kwenye makaburi ya watu wasio kuwa na ndugu, tukashangaa kuona mbwa takribani sita wakiwa juu ya makaburi wakila viungo vya binadamu”,anaeleza Joseph.
“Tuliona mifupa tu ya mbavu,hatukuona utumbo lakini kwenye kaburi moja kulikuwa na vipande vingine vya mwili vikiwa vimefunikwa na mfuko wa sandarusi vikivuja damu huku kukiwa na harufu mbaya”,anaongeza Joseph.
Kwa upande wao wajumbe wa serikali ya mtaa wa Mageuzi kata ya Ngokolo yalipo makaburi hayo Mhoja Pius na Sada Bakari wameeleza kusikitishwa kitendo cha uzembe wa halmashauri ya manispaa ya Shinyanga kutosimamia vizuri mazishi ya watu wasiokuwa na ndugu.
“Haiwezekani kaburi la binadamu liwe na urefu wa futi moja halafu inavyoonekana watu zaidi ya mtu mmoja wamezikwa katika kaburi moja, hili tukio la miili ya binadamu kufukuliwa ni la pili jingine lilitokea mwaka 2012 tulikuta mtu kazikwa huku mkono wake ukiwa nje ya kaburi”,wamesema
Nao wakazi wa eneo hilo Jofrey Rugalema na Onesmo Omari wanasema…
“Tunalaani kitendo hiki cha kinyama,tunautaka uongozi wa manispaa ya Shinyanga kuthamini binadamu hata kama hawana ndugu …ni fedheha kubwa mizoga ya binadamu kuokotwa mtaani…usimamizi wa mazishi ya watu wasio na ndugu ni mbovu,kinachokera zaidi pamoja na kupigiwa simu hakuna hata kiongozi mmoja wa manispaa aliyefika katika eneo la tukio..polisi pakee ndiyo wamekuja”,wamesema.
Malunde1 blog imemtafuta mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Lewis Kalinjuna kuzungumzia tukio hilo lakini mpaka sasa simu yake haipatikani.
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Mika Nyange ameiambia Malunde1 blog kuwa baada ya kupata taarifa za kuwepo kwa tukio hilo wamefika eneo la tukio na kubaini kuwa makaburi hayo yamefukuliwa na fisi na kwamba kwa mujibu wa sheria na taratibu manispaa ndiyo wahusika na wanatakiwa washirikiane na wananchi kuzika upya miili ya marehemu.
Vipande vya mwili wa binadamu vilivyookotwa katika mtaa wa Butengwa kata ya Ndembezi jirani na makaburi ya mtaa wa Mageuzi yaliyopo katikakata ya Ngokolo katika manispaa ya Shinyanga-Picha na Kadama Malunde-Malunde1 blog
Kushoto ni vipande vya nyama zinazodaiwa kuwa kuwa ni vya binadamu,kulia ni mojaya makaburi mawili yaliyofukuliwa,kinachoonekana ni vipande vya mwili wa binadamu vikiwa vimefunikwa mfuko wa sandarusi katika makaburi ya Mageuzi yaliyopo katika kata ya Ndembezi katika manispaa ya Shinyanga
Wananchi wakioneshana kaburi jingine lililofukuliwa,ambapo ndani kulikuwa na mfupa uliokauka
Viungo vya binadamu vikiwa kaburini
Wananchi wakifukia makaburi hayo
Mifupa inayodaiwa kuwa ni ya binadamu iliyookotwa kwenye makaburi hayo
Mwananchi akiwa amebeba vipande vya mifupa kwenye koleo
Wananchi wakiendelea kuokota mifupa makaburini
Mfupa ukiwa kwenye majani makaburini
Wananchi wakiondoka makaburini baada ya kuzika/kufunika miili ya binadamu kwenye makaburi yaliyokuwa wazi
Viongozi wa mtaa wa Mageuzi na Butengwa na wananchi wakitafakari jambo makaburini
Kushoto ni mjumbe wa serikali ya mtaa wa Mageuzi kata ya Ngokolo yalipo makaburi hayo Mhoja Pius akisikiliza kwa makini maelezo kutoka kwa mjumbe wa serikali ya mtaa wa Butengwa Peter Joseph ambako vipande vya miili ya binadamu imeokotwa
Mjumbe wa serikali ya mtaa wa Mageuzi kata ya Ngokolo yalipo makaburi hayo Mhoja Pius akizungumza na Malunde1 blog
Kushoto ni mjumbe wa serikali ya mtaa wa Mageuzi kata ya Ngokolo yalipo makaburi hayo Mhoja Pius akiteta jambo na mjumbe wa serikali ya mtaa wa Butengwa Peter Joseph ambako vipande vya miili ya binadamu imeokotwa
Mkazi wa eneo hilo Onesmo Omari akielezea kuhusu tukio hilo
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog
Chapisha Maoni