HOME
Fedha za Escrow pasua kichwa
SAKATA
la namna fedha za Akaunti ya Escrow zilivyotolewa Benki Kuu ya Tanzania
limeendelea kuibuka, ambapo malipo yanayalolamikiwa kufanywa na benki
hiyo kwa Kampuni ya Independent Power Limited (IPTL), imeelezwa ni
halali kwani si fedha za umma.
Mwanasheria na Katibu wa IPTL na Kampuni ya Pan African Power (PAP), Joseph Makandege, alisema akaunti hiyo ilifunguliwa kwa makubaliano baina ya IPTL na Serikali, ambapo BoT ilichaguliwa kama wakala wa kutunza fedha.
Alisema hali hiyo ilitokana na kuwepo kwa mgogoro wa kimaslahi baina ya wabia wa IPTL, ambao ni Kampuni ya VIP (ambayo ilikuwa inamiliki asilimia 30 ya hisa) na inamilikiwa na James Rugemarila na kampuni ya Mechmar kutoka Malaysia, ambayo ilikuwa ikimiliki asilimia 70.
Katibu alisema taarifa zilizopo katika nyaraka zinaonesha Mahakama Kuu iliamua pande zote mbili VIP na Mechmar zisaini hati ya makubaliano ya namna ya kutunza fedha za malipo ya kila mwezi za umeme, ambayo IPTL inauzia Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco).
"Nyaraka hizo zinaonesha Mahakama ilielekeza kuwa malipo hayo yahifadhiwe katika akaunti maalumu hadi mgogoro utakapoamriwa baina ya wabia hao, ambapo kwa pamoja wabia hao walikubaliana kufungua akaunti ya pamoja katika Benki Kuu ya Tanzania na akaunti hiyo kuitwa Escrow.
"Taarifa katika nyaraka hizo ilionesha BoT alikuwa kama wakala wa kutunza fedha hizo, ambapo Tanesco na Serikali nao walisaini hati kama sehemu ya wabia, ambapo wao wakiwa walipaji wa umeme kwa IPTL.
"Kwa mujibu wa nyaraka hizo, makubaliano hayo yalifikiwa Julai 5, 2006, huku kila upande ukiwakilishwa na wahusika na kutia saini hizo, ambapo kwa upande wa Serikali alisaini aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini kwa wakati huo, Arthur Mwakapugi," alisema.
Mwanasheria huyo aliongeza kuwa, "taarifa hiyo ilionesha kwa upande wa IPTL, alisaini aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Datuk Baharuden Majid na upande wa BoT, alisaini aliyekuwa Gavana, Daudi Balal (marehemu), kama wakala wa kuhifadhi fedha hizo.
Makandege alisema Watanzania wataendelea kuelewa ukweli halisi polepole kuhusiana na akaunti hiyo. Alisema mengi yanayoenezwa kuhusiana na IPTL si kweli, kwa kuwa malipo waliyopewa na BoT ni halali na malipo hayo yalifanyika baada ya mgogoro wa pande mbili za wabia kumalizika

Chapisha Maoni