HOME
Bill Gates kwenye huu mradi wa maji yanayotokana na taka za binadamu!
Mmiliki wa kampuni ya Microsoft Corporation, Bill Gates ameendelea kuuthibitishia ulimwengu kwamba haogopi kuwekeza pesa yake kwenye biashara yoyote Duniani.
Ni
mmoja ya watu wanaofadhili miradi mikubwa ya kilimo Afrika, leo kuna hii
story ambayo kama ingekuwa Bongo mtu anawekeza upande huu ni wachache
ambao wangemuunga mkono.
Picha na video zimeenea mitandaoni, Gates kaamua kugeukia huu mradi wa maji safi ya kunywa ambayo yametengenezwa kutokana na kinyesi cha binadamu.
Mikakati
ya Gates ni kushirikiana na Kampuni hiyo kusambaza mitambo hiyo katika
nchi mbalimbali maskini ikiwemo Senegal muda mfupi baada ya majaribio
yake kukamilika.
Teknolojia hiyo imeungwa mkono na shirika la WaterAid
ambalo limesema kuwa litasaidia sana katika maeneo ya mengi yenye ukame
ambapo kulingana na shirika hilo watu millioni 748 hawana maji safi ya
kunywa.
Video iliyowekwa katika blog yake, Bill Gates
alishuhudia hatua zote, kuanzia kinyesi cha binadamu kikiingizwa katika
mtambo huo mpaka maji yalipotoka na akayanywa baada ya kupitia hatua
zote za utayarishaji.
Cheki video hii inayoonyesha mfumo mzima wa maji hayo yanavyoandaliwa kutoka kwenye mfumo wa taka.
Chapisha Maoni