Unknown Unknown Author
Title:
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
HOME Rambo kutengeneza filamu tatu mwaka 2015. . Mkali wa Movie za matukio ya mapigano au Action Movies Sylvester Stallone a...
HOME

Rambo kutengeneza filamu tatu mwaka 2015.

john-rambo-wallpapers-2026x1500

Mkali wa Movie za matukio ya mapigano au Action Movies Sylvester Stallone ametangaza ujio wa filamu yake mpya itakayokuwa sehemu ya mwisho ya mfululizo wa filamu za Rambo ambazo zimemjengea umaarufu kiasi cha watu kumpachika jina la Rambo.
Stallone alithibitisha habari hizi kutumia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa twitter ambapo alikuwa akizungumza na mashabiki wake ambao aliwaambia kuwa sehemu ya miwhso ya filamu za Rambo itaanza kutengenezwa  mwaka huu .
Filamu hii ambayo itapewa jina la Rambo The Last Blood inamuonyesha mkongwe wa vita ya Vietnam John Rambo akiwa kwenye harakati zake za mapambano na filamu hii haitakwenda mbali na story ya filamu hizi ambazo sehemu yake ya kwanza iliigizwa mwaka 1982 katika filamu iliyoitwa Rambo First Blood .
Moja ya taswira za kukumbukwa kwenye filamu ya kwanza ya Joh Rambo First Blood.
Moja ya taswira za kukumbukwa kwenye filamu ya kwanza ya Joh Rambo First Blood.
Mwaka 2015 unatarajiwa kuwa mwaka ambao Stallone atakuwa ‘Busy’ akitengeneza filamu tatu tofauti ikiwemo Scarpa ambayo ataanza kuitengeneza mara tu baada ya Rambo Last Blood kumalizika na pia anatarajia kutengeneza sehemu nyingine ya filamu za Rocky Balboa ambapo safari hii ataigiza kama kocha wa mjukuu wa mpinzani wake wa zamani ulingoni Apolo Creed.
Hii ni moja ya sehemu zilizoonekana kwenye mfululizo wa filamu za Rocky ambapo Sylvester Stalone ameigiza kama bondia.
Hii ni moja ya sehemu zilizoonekana kwenye mfululizo wa filamu za Rocky ambapo Sylvester Stalone ameigiza kama bondia.
Rambo ambaye ana umri wa miaka 68 amesema kuwa amelazimika kufanya mazoezi makali ili kutengeneza mwili wake kuendana na uhusika wa sehemu atakazokuwa akiigiza ili aweze kuendana na story halisi zilizomo kwneye filamu hizi hasa ukizingatia kuwa filamu anazotengeneza ni za mapigano na utimamu wa mwili na matumizi ya nguvu nyingi ni jambo la lazima .

Stallone ana umri wa miaka 68 na bado anaendelea kufanya filamu za Action.
Stallone ana umri wa miaka 68 na bado anaendelea kufanya filamu za Action.

Mwaka huu Sylvester Stallone atafanya filamu tatu tofauti.
Mwaka huu Sylvester Stallone atafanya filamu tatu tofauti.

About Author

Advertisement

Chapisha Maoni

 
Top