HOME
Katibu
wa kamati maalum ya NEC, idara ya itikadi na uenezi CCM Zanzibar Bi,
Waride Bakar Jabu akimkabidhi misaada Katibu mkuu wa ofisi ya makamo wa
pili wa rais, Joseph Abdallah Meza kwa ajili ya kuwasaidia wahanga wa
mafuriko waliopo kambi ya mwanakwere "C" Unguja.
Katibu
wa kamati maalum ya NEC, idara ya itikadi na uenezi CCM Zanzibar Bi,
Waride Bakar Jabu akikagua wahanga wa mafuriko katika kambi ya
mwanakwere zanzibar.
Kambi ya kipindupindu iliyopo chumbuni Zanzibar.
CHAMA
chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar kimewataka wananchi kuendelea kufuata
kanuni na taratibu zinazotolewa na wataalamu wa kiafya ili kujikinga
na maambukizi ya maradhi ya kipindupindu yaliyopo nchini.
Wito
huo umetolewa na Katibu wa Kamati Maalum NEC, Idara ya Itikadi na Uenezi
CCM Zanzibar, Waride Bakar Jabu katika ziara ya kuwatembelea na
kuwafariji wagonjwa wa Kipindupindu wa kambi iliyopo Chumbuni Zanzibar,
alisema endapo wananchi watafuata kanuni za kiafya itasaidia kutoweka
ugonjwa huo kwa haraka.
Waride
alisema CCM itaendelea kutoa misaada ya hali na mali kwa wagonjwa wa
kipindupindu ili kusaidia serikali huduma za uendeshaji kwa wagonjwa
hao.
“
Tunawaomba wananchi waendelee kuweka mazingira yao katika hali ya usafi
sambamba na kutumia maji salama, vyoo kuwa visafi na wagonjwa wenye
dalili za maradhi hayo kupelekwa haraka katika kambi za kipindupindu.
Pia
CCM inawapa pole wananchi wote waliopata maradhi ya kipindupindu na
kuwasihi waendelee kuwa wavumilivu katika kipindi hiki kigumu cha
matibabu yao.”, alisema Bi, Waride na kuzisihi taasisi zingine za
serikali na binafsi kutoa misaada kwa wagonjwa hao kwani maradhi ya
Kipindupindu hayana itikadi za kisiasa bali yanawapata wananchi wote.
Aliwashauri
wanawake nchini ambao ni walezi wa watoto na mama wa nyumbani kuacha
tabia ya kutupa ovyo pempasi za kuwafungia watoto kwani nazo ni miongoni
mwa vitu vinavyopelekea kuenea kwa maradhi ya kipindupindu nchini.
“
Wanawake tukumbuke kuwa kila janga lolote sisi pamoja na watoto ndiyo
waathirika wa mwanzo hivyo lazima tuwe makini katika kuweka mazingira
yetu katika hali ya usafi pia tusitupe pempasi ovyo bali tuziweke katika
sehemu zinazostahiki.” Alisisitiza Waride.
Naye
Daktari dhamana wa Wilaya ya Magharibi Unguja ambaye pia ni Mkuu wa
Kambi ya Kipindupindu Chumbuni Zanzibar, Ramadhan Mickdad Suleiman
ameshukru msaada uliotolewa na CCM na kuahidi kuutumia kwa malengo
yaliyokusudiwa.
Akitoa
takwimu za hali ya maambukizo ya ugonjwa huo kwa sasa, Mickdad alisema
ya hali ya maambukizo kwa sasa imepungua kutoka wagonjwa 40 kwa siku
hadi 21 wanaolazwa katika kambi hiyo.
Alisema
hali hiyo imetokana na utekelezaji wa agizo la Rais wa Zanzibar Dkt.
Ali Mohamed Shein alipowaagiza wananchi wanaofanya biashara za vyakula
na vinywaji kuacha kuuza kwa muda ili kudhibiti kupunguza kasi ya
maambukizi ya kipindupindu.
Alifafanua
kuwa mpaka sasa kambi hiyo tayari imeshapokea wagonjwa 2026 waliopatiwa
matibabu na kupona na wakaondoka na kati ya hao wamefariki wagonjwa 43
mpaka sasa.
“
Tunaishauri jamii kudumisha usafi wa vyoo na kula vyakula na maji
vilivyokuwa salama kwani ugonjwa huu unaambukizwa kwa kasi katika maji
ya kunywa yenye bakteria wa kipindupindu ama kumgusa maiti yaliyekufa
kwa ugonjwa au kugusana na mtu aliyeambukizwa kipindupindu.”, alisema
Bi, Micjdad.
Aliwaomba
wananchi wenye uwezo pamoja taasisi binafsi na serikali kutoa misaada
kujitokeza kutoa misaada mbali mbali ya kuwasaidia wagonjwa wa maradhi
hayo waliopo katika kambi hiyo.
Mapema
Waride alitembelea na kuwafariji Wahanga wa mafuriko waliopo katika
kambi ya Shule ya Mwanakwerekwe “ C” Unguja, aliwapa pole kwa matatizo
yaliyowafika na kuwaomba waendelee kuwa wavumilivu katika kambi hili
huku serikali ikiendelea kutafuta mbinu za kuwasaidia ili wapate makaazi
katika sehemu salama.
Alitoa
wito kwa wananchi wanaoishi katika sehemu za mabonde na sinazojaa maji
wakati wa msimu wa mvua za maska kuhama haraka kabla hawajapata athari
za kukumbwa na mafuriko hayo.
Kwa
upande wake Katibu mkuu wa Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Zanzibar,
Joseph Abdallah Meza alitoa shukrani kwa uongozi wa CCM kwa msaada wao
wa kuisaidia kambi hiyo yenye wananchi zaidi 400.
Alisema
serikali bado inaendelea kuwahudumia wananchi hao ambao wamepata maafa
ya mafuriko na kupoteza makaazi yao hivyo bado panahitajika misaada
mbali mbali ya maji na vyakula pamoja na huduma za kibinadamu.
Misaada
iliyotolewa na CCM katika ziara hiyo ina thamani zaidi ya shilingi
milioni tano (5) kwa upande wa kambi ya kipindupindu Chumbuni ni pamoja
na Maji ya kunywa, Dawa za Chroline, Sabuni za kufulia na kuogea, viatu
vya mvua, dawa ya choo na mashine za kufukizia dawa Sprayers.
Vingine
vilivyotolewa katika kambi ya wahanga wa mafuriko iliyopo Mwanakwere
“C” ni pamoja na Pempasi za watoto, maji ya kunywa, sabuni za kuogea na
kufulia, sabuni za chooni na madaftari ya wanafunzi.
Chapisha Maoni