HOME
Kamishna
Jenerali wa Magereza nchini, CGP John Casmir Minja katika jukwaa
akipokea salaam ya heshima kutoka Gadi Maalum iliyoandaliwa na Maofisa
Wahitimu wa Mafunzo ya Maafisa Wateule Daraja la Kwanza(hawapo pichani).
Kamishna
Jenerali wa Magereza nchini, CGP John Casmir Minja akikagua Gadi Maalum
iliyoandaliwa na Maofisa Wahitimu wa Mafunzo ya Maafisa Wateule Daraja
la Kwanza yalifanyika Aprili 27, 2016 katika Viwanja vya chuo cha Jeshi
la Magereza, KPF Mkoani Morogoro.
Kamishna
Jenerali wa Magereza nchini, CGP John Casmir Minja(kushoto) akimvisha
cheo cha RSM mmoja wa Wahitimu wa Mafunzo ya Maafisa Wateule Daraja la
Kwanza ambaye amefanya vizuri zaidi katika Mafunzo hayo yaliyofanyika
kwa muda wa miezi miwili.
Baadhi
ya Maofisa wa Kike wa Jeshi la Magereza ambao ni miongoni mwa wahitimu
wa Mafunzo ya Maafisa Wateule Daraja la Kwanza kama wanavyoonekana
katika picha.
Kamishna
Jenerali wa Magereza nchini, CGP John Casmir Minja akitoa hotuba fupi
kwa Wahitimu wa Mafunzo ya Maafisa Wateule Daraja la Kwanza(hawapo
pichani).
Maofisa
Wahitimu wa Mafunzo ya Maafisa Wateule Daraja la Kwanza wakifuatilia
kwa makini hotuba ya mgeni kama wanavyoonekana katika picha.
Kamishna
Jenerali wa Magereza nchini, CGP John Casmir Minja akifanya mahojiano
na baadhi ya Wawakilishi wa Vyombo vya Habari, Mkoani Morogoro.
Kamishna
Jenerali wa Magereza nchini, CGP John Casmir Minja(katikati) akiwa
katika picha ya pamoja na Maofisa Wahitimu wa Mafunzo ya Maafisa Wateule
Daraja la Kwanza waliosimama mstari wa nyuma.
(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).
Chapisha Maoni