Na Rabi Hume, MoDewjiBlog
Kwa
kuhakikisha jamii inakuwa katika hali ya usalama wa kiafya, Taasii ya
Fazel Foundation kwa kushirikiana na Taasisi ya Elimu ya Afya na Madawa
(TAHMEF) wametoa huduma ya upimaji wa magonjwa mbalimbali kwa wananchi
wa Kigogo, Dar es Salaam.
Zoezi
hilo lilifanyika Aprili, 23 katika Msikiti wa Al Ghadir uliopo Kigogo
Post na jumla ya 352 wanawake wakiwa 150 na wanaumme 202 walipimwa
Malaria, Kisukari, Shinikizo la Damu na Upungufu wa Damu mwilini.
Kati
ya watu hao, watu 38 wameonekana kuwa na Shinikizo la Damu, 36 Upungufu
wa Damu, 8 Kisukari na mmoja Maralia ambapo walipata nafasi ya kupatiwa
dawa na ushauri kutoka kwa madaktari mbalimbali.
Aidha
kwa mafanikio hayo, Fazel Foundation inawashukuru wote walioshiriki
katika huduma hiyo akiwepo Dkt. Mohammed Alloo, Dkt. Sibtain Moledina,
Mohammed Enterprises Tanzania Limited (METL Group), Salama
Pharmaceuticals na Clinicheck Labs, Imam wa msikiti wa Al Ghadir Sheikh
Jalala, Msikiti wa Al Ghadir, Diwani wa Kigogo, Bw. Manyama, Team ya
Volunteers na Hawza ya Imam Sadiq kwa ushiriki wao katika zoezi hilo.
Mwanzilishi
wa Taasisi ya Fazel, Dkt. Sajjad Fazel akisalimiana na Diwani wa
Kigogo, Bw. Manyama wakati wa funguzi wa huduma ya upimaji wa afya bure
kwa wakazi wa Kigogo. Katikati ni Imam wa Msikiti wa Al Ghadir , Sheikh Jalala. (Picha zote na Rabi Hume - modewjiblog.com)
Wakiwa
katika picha ya pamoja, Wa kwanza kushoto ni Diwani wa Kigogo, Bw.
Manyama, Imam wa Msikiti wa Al Ghadir , Sheikh Jalala, Mwanzilishi wa
Taasisi ya Fazel, Dkt. Sajjad Fazel na Mwanzilishi wa Taasisi ya Elimu
ya Afya na Madawa (TAHMEF), Juliana Busasi.
Boniventure
Pius akimpima Imam wa Msikiti wa Al Ghadir, Sheikh Jalala wakati wa
uzinduzi wa upimaji afya bure kwa wakazi wa Kigogo. Aliyesimama kulia ni
Mwanzilishi wa Fazel Foundation, Dkt. Sajjad Fazel.
Mkisi
Shamra akimuhudumia mmoja wa wananchi waliofika katika kituo
kilichokuwa kikitumika kupima afya bure kwa wakazi wa Kigogo, Dar es
Salaam.
Mary
Kalleku akimpima mmoja wa wananchi waliofika katika kituo kilichokuwa
kikitumika kupima afya bure kwa wakazi wa Kigogo, Dar es Salaam.
Victoria
Msambichaka akimwambia jambo mmoja wa wananchi waliofika katika kituo
kilichokuwa kikitumika kupima afya bure kwa wakazi wa Kigogo, Dar es
Salaam.
Baadhi ya wananchi waliofika kupimwa afya bure kutoka Fazel Foundation na TAHMEF.
Eneo lililokuwa likitumika kupokea wananchi waliokwenda kupima bure afya zao.
Dkt.
Mohammed Alloo kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili akimshauri jambo
mmoja wa wananchi waliofika katika kituo kilichokuwa kikitumika kupima
afya bure kwa wakazi wa Kigogo, Dar es Salaam.
Alex Juma akimpa dawa mmoja wa wananchi aliyefika kupima afya bure baada ya kubainika kuwa na ugonjwa.
Mwanzilishi
wa Fazel Foundation, Dkt. Sajjad Fazel akizungumza jambo na Mwanzilishi
wa Taasisi ya Elimu ya Afya na Madawa (TAHMEF), Juliana Busasi wakati
wakati zoezi la kupima afya bure kwa wakazi wa Kigogo likiendelea.
Kenneth
Mananu akimsikiliza mmoja wa wananchi waliofika kituoni kupata vipimo
vya afya bure. Anayefuatia ni Joshua Mnkeni akimpa ushauri mmoja wa
wananchi aliyefika kupata huduma ya kupima afya bure.
Eneo la kutolea huduma kwa wananchi wanaofika kupata huduma.
Wagonjwa wakisubiri kumuona daktari.
Hans Olomi akimpima mmoja wa watoto waliofika kupimwa afya zao bure, Anayefuatia ni Simon Nassary.
Mwanzilishi wa Fazel Foundation, Dkt. Sajjad Fazel akimwambia jambo Kenneth Munanu wakati zozi la upimaji likiendeea.
Chapisha Maoni