Mbunge wa Jimbo la Mikumi Joseph Haule a.ka Profesa Jay April 25 2016 siku moja baada ya kupeleka msaada wa mabomba Ruaha
amelazimika kwenda kuwatembelea wanakijiji wa Changalawe kata ya
Masanze ambao wamepata mafuriko na baadhi ya mali zao kwenda na maji.
Prof Jay
ameenda kuwatembelea wakazi hao ambao mazao yao yameenda na maji
mashambani pamoja na nyumba zao kusombwa na mafuriko, mbunge huyo wa Mikumi hakuishia kutoa pole tu lakini amehaidi kuwapelekea msaada ili kuwapunguzia matatizo yaliojitokeza katika mafuriko hayo.
Chapisha Maoni