HOME
Brasbendi
ya Chipkizi ikiongoza matembezi ya wauguzi yakipita katika maeneo ya
Kisonge kuelekea Studio za Rahaleo ambapo sherehe hizo ziliadhimishwa
rasmi.
Waandamanaji wakiingia kwa furaha eneo la Studio za Rahaleo ambapo sherehe za sikuya Waguzi Duniani ziliadhimishwa.
Mrajis
Baraza la Wauguzi na Wakunga Zanzibar Vuai Kombo Haji akiongoza kiapo
cha wauguzi katika maadhimisho ya siku ya wauguzi Duniani yaliyofanyika
Ukumbi wa Sanaa Rahaeo.
Mkurugenzi
Tiba Katika Wizara ya Afya Dkt. Salhia Ali Muhsin akimkaribisha mgeni
rasmi Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo aliemwakilishi Mke wa Rais wa
Zanzibar Mama Mwanamwema Shein katika maadhimisho hayo.
Baadhi
ya wauguzi walioshiriki maadhimisho hayo wakifuatilia hotuba zilizokuwa
zikitolewa katika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo, Mjini Zanzibar.
Waziri
wa Afya Mhmoud Thabit Kombo aliemuwakilisha Mke wa Rais wa Zanzibar
akisoma hotuba katika maadhimisho ya siku ya wauguzi Duniani
yaliyofanyika Ukumbi wa Sanaa Rahale Mjini Zanzibar.
Picha
ya pamoja ya baadhi ya viongozi wa wauguzi na Mgeni rasmi, Waziri wa
Afya Mhmoud Thabit Kombo. Picha na Makame Mshenga Maelezo Zanzibar.
Muhimbili Kutoa Tiba Wagonjwa wa Homa Sugu ya Ini.
Mtaalamu
kutoka Marekani, Dk Brian McMahon akizungumza na madaktari na wauguzi
wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) kuhusu tiba ya homa sugu ya ini
inayosababishwa na virusi vya Hepatitis B.
Dk
Aaron Haris kutoka Marekani akielezea jinsi mradi huo
utakavyowanufaisha Watanzania ambao wameambukizwa virusi vya vya
Hepatitis B.
Madaktari na wauguzi wakimsikiliza Dk McMahon wakati akielezea kuanza kwa mradi wa tiba ya homa ya ini kwa watu mbalimbali.
Mkuu
wa Idara ya Magonjwa ya Tumbo, Dk John Rwegasha (kushoto) akifuatilia
mada iliyowasilishwa na Dk Edwin Masue na Dk Eva Uiso wa Hospitali ya
Taifa ya Muhimbili. Wengine ni Dk McMahon na Dk Haris kutoka Marekani.
Dk
Edwin Masue wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) akiwasilisha mada
kuhusu dalili za homa sugu ya ini inayosababishwa na virusi vya
Hepatitis B.
Picha zote na John Stephen, Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).
Na Neema Mwangomo-MNH.
Hospitali
ya Taifa Muhimbili-MNH-inatarajia kuanza kampeni ya kupima na kutoa
tiba kwa ugonjwa wa Homa Sugu ya Ini ambao unasababishwa na Virusi
vya HEPATITIS B .
Daktari
Bingwa wa magonjwa ya Mfumo wa Chakula na Ini katika Hospitali ya
Taifa Muhimbili, Edwin Masue amesema kundi la ndio limeonekana
kuathirika zaidi kwa kuwa mtoto anapata maambukizi kutoka kwa mzazi .
Kwa
mujibu wa Dk. Masue mtoto anapozaliwa lazima apatae chanjo, na pia mama
mjamzito ambaye anagundulika kuwa ana Virusi vya HEPATITIS B hupatiwa
dawa ya kumkinga mtoto katika miezi mitatu ya mwisho kabla ya
kujifungua .
“Tuangalie
uwezekano ili watu waelewe tatizo hili mapema , wapime na wawahi kupata
matibabu kwani maambukizi makubwa yanatoka kwa mama kwenda mtoto na
kwa wale wanaoanza kutumia dawa za VVU wanatakiwa kupima ugonjwa wa homa
ya Ini kwa kuwa virusi vinaingiliana,” amesema Dk . Masue .
Mkakati wa MHN.
Kwa
upande wake Daktari John Rwegasha amesema katika kipindi cha Julai mwaka
huu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kutaanzishwa mradi wa miaka
mitano ambao unalenga kupima na kutibu watu ambao watagundulika kuwa na
homa sugu ya ini na kwamba hata baada ya kukamilika kwa mradi huo
wananchi wataendelea kupatiwa matibabu bure.
“
Kuna muongozo wa tiba wa Shirika la Afya Duniani-WHO- ambao umetolewa
mwaka jana hivyo tunataka kuangalia matumizi ya huo muongozo kwenye nchi
zetu za Dunia ya tatu , kuna watu wametusaidia tulikuwa hatuna uwezo wa
dawa. Awali tulikuwa tunaazima dawa kwenye mradi wa HIV hivyo kupitia
mradi huo tutakuwa na dawa pamoja na vitenganishi vya kimaabara,”
amesema Dk Rwegasha.
“Kati
ya watu 100, wanane wanatembea na ugonjwa huo bila kufahamu baada ya
miaka 20 mtu anapata matatizo ya ini na kusababisha ini kushindwa
kufanya kazi na tumbo kuvimba hivyo natumia fursa hii kuwaambia
wananchi wajitokeze kupima mapema ili waweze kupatiwa matibabu,”
amesema.
Virusi vinavyoenea:
Kwa
mujibu wa watalaam , asilimia kubwa ya Virusi vya HEPATITIS B vipo
kwenye damu , mbegu za kiume , ute wa mwanamke na hedhi ya mwanamke na
kwamba maambukizi yake hayana tofauti na maambukizi ya Virusi vya
Ukimwi.
Dalili za ugonjwa huo:
-Kichefuchefu
-Kukosa hamu ya kula
-Macho kua ya njano
-Mkojo kuwa wa njano
-Kupata choo chenye rangi ya njano ambayo imepauka
-Mwili mzima kuishiwa nguvu.
Hata hivyo dalili hizo si zote zinaenda pamoja , kuna wengine huwa hawana dalili hizo kabisa.
Chapisha Maoni