HOME
|
Ni
katika siku ya pili ya mafunzo kwa waandishi wa habari mkoa wa
Shinyanga juu ya tohara ya wanaume iliyokuwa inafanyika mjini Kahama
Agosti 21 na 22,2014 ambapo mbali na kujifunza mambo kadhaa kuhusu
tohara ya wanaume waandishi hao pia wamepata fursa ya kutembelea baadhi
ya vituo vinavyotoa huduma hiyo wilayani Kahama.
Mafunzo/Kampeni
hizo za tohara ya mwanaume zinaendeshwa kwa ushirikiano kati ya
serikali ya Tanzania na Mradi wa kuzuia UKIMWI wa IntraHealth kwa
ufadhili/unaofadhiliwa na Mfuko wa Rais wa Marekani wa Kudhibiti UKIMWI
na Taasisi ya Tiba na Kinga dhidi ya Maradhi ya Marekani CDC. Pichani ni Mwezeshaji
wa mafunzo ya Tohara ya wanaume kitaifa kutoka wilaya ya Itilima mkoani
Simiyu Dkt Nicholaus Mbassa akimfanyia huduma mmoja wa wanaume
waliofika katika kituo cha tohara ya wanaume katika hospitali ya wilaya
ya Kahama leo |
|
Lydia
Mabagala,mmoja kati ya wahudumu wa tohara ya wanaume katika kituo cha
tohara ya wanaume/kliniki ya wanaume katika hospitali ya wilaya ya
Kahama mkoani Shinyanga akizungumza na waandishi wa habari waliofika
kituoni hapo leo kushuhudia namna shughuli ya tohara ya wanaume
inavyofanyika,ikiwa ni katika mafunzo yaliyoandaliwa na shirika la
Intrahealth kwa kushirikiana na serikali kuwajengea uwezo katika
kuripoti habari zinazohusiana na tohara ya wanaume kama njia ya
kujikinga na maambukizi ya VVU |
|
Hapa
ni katika Zahanati ya wazazi Nyandekwa/kituo cha tohara ya
wanaume/kliniki ya tohara ya wanaume Nyandekwa iliyopo katika
halmashauri ya mji Kahama ambapo waandishi wa habari waliopatiwa mafunzo
ya tohara wametembelea.Pichani vi vifaa vinavyotumika katika tohara ya
wanaume |
|
Hawa
ni vijana kutoka kata ya Nyandekwa waliohamasika na kuamua kufika
katika kliniki ya tohara ya wanaume ya Nyandekwa kwa ajili ya kufanyiwa
tohara.Kampeni
hizo za tohara ya mwanaume zinaendeshwa kwa ushirikiano kati ya
serikali ya Tanzania na Mradi wa kuzuia UKIMWI wa IntraHealth kwa
ufadhili/unaofadhiliwa na Mfuko wa Rais wa Marekani wa Kudhibiti UKIMWI
na Taasisi ya Tiba na Kinga dhidi ya Maradhi ya Marekani CDC. |
|
Kushoto
ni Nchama Samson, mmoja wa watoa huduma ya tohara ya wanaume
katika kliniki ya tohara ya wanaume ya Nyandekwa akizungumzia zoezi
zima la tohara katika kituo hicho ambapo alisema kila siku wanaume zaidi
ya 40 hufika kituoni hapo kwa ajili ya huduma ya tohara,kulia kwake ni
afisa mtendaji wa kata ya Nyandekwa bwana Kintoki Musiba |
|
Waandishi
wa habari wakisikiliza maelezo kutoka kwa Nchama Samson, mmoja wa watoa
huduma ya tohara ya wanaume katika kliniki ya tohara ya wanaume ya
Nyandekwa
|
Nchama
Samson, mmoja wa watoa huduma ya tohara ya wanaume katika kliniki ya
tohara ya wanaume ya Nyandekwa akiendelea kutoa maelezo |
|
|
Kundi
kubwa la wanaume waliofika katika kliniki ya tohara ya wanaume ya
Nyandekwa wakizungumza na waandishi wa habari ambapo walisema hivi sasa
wanaelewa faida ya kufanyiwa tohara ndiyo maana wanajitokeza kwa wingi
ili kujikinga na VVU na magonjwa mengine |
|
Mazungumzo ya waandishi wa habari na wanaume yakiendelea |
|
Kulia
ni mzee Hassan Saidi kutoka kijiji cha Nyandekwa aliyeleta kijana wake
kufanyiwa huduma ya tohara akizungumza na waandishi wa habari
leo,kushoto kwake ni afisa mtendaji wa kata ya Nyandekwa bwana Kintoki
Musiba |
|
Kushoto ni Mwezeshaji
wa mafunzo ya Tohara ya wanaume kitaifa kutoka wilaya ya Itilima mkoani
Simiyu Dkt Nicholaus Mbassa,wa pili kushoto ni bwana Christopher
Anjelo aliyefika kituoni hapo kwa ajili ya kufanyiwa tohara leo,mbele ni
mwandishi wa habari TBC bwana Grayson Kakuru wakiwa eneo la kituo cha
tohara ya wanaume Nyandekwa |
|
Kulia
ni afisa mtendaji kijiji cha Nyandekwa bwana Andrew Maganga akiwa na
vijana waliofika katika kituo hicho kufanyiwa tohara.Alisema wamekuwa
wakiwatumia viongozi wa vitongoji na walimu katika kuhamasisha wanaume
kufanyiwa tohara |
Darasa la Tohara kwa wanaume/vijana-Nchama Samson, mmoja wa watoa huduma ya tohara ya wanaume katika kliniki
ya tohara ya wanaume ya Nyandekwa akitoa elimu kuhusu Tohara kwa
wanaume/vijana waliofika kituoni hapo kwa ajili ya tohara kabla ya
kufanyiwa tohara.
|
Darasa linaendelea,kabla ya kufanyiwa tohara unaelimishwa kwanza |
Baada
ya kutembelea kituo cha Nyandekwa baadhi ya waandishi wa habari
waliohudhuria mafunzo ya tohara ya wanaume wakiwa katika pozi nje ya
kituo hicho
BOFYA HAPA KUONA KILICHOJIRI SIKU YA KWANZA YA SEMINA YA TOHARA KWA WAANDISHI WA HABARI MJINI KAHAMA
VIA KADAMA MALUNDE
Chapisha Maoni