HOME
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imetoa onyo pamoja na kutoza faini ya takribani Sh milioni 5 kwa kituo cha redio na televisheni cha Clouds, kwa kukiuka kanuni za utangazaji za mwaka 2005.
Uchawi, Safari za Kuzimu na maswali ya Aibu kwa washiriki wa Bibi Bomba Vyaiponza Clouds FM na Clouds TV.....TCRA Yawalima faini
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imetoa onyo pamoja na kutoza faini ya takribani Sh milioni 5 kwa kituo cha redio na televisheni cha Clouds, kwa kukiuka kanuni za utangazaji za mwaka 2005.
Wakielezea
uamuzi huo jana jijini Dar es Salaam, Kamati ya Maudhui ya mamlaka
hiyo ikiongozwa na Mwenyekiti wake, Margaret Munyagi ilisema kuwa
ukiukwaji wa kanuni hizo ulifanywa kwa nyakati tofauti na vituo hivyo.
Alisema
kwa upande wa kituo cha redio cha Clouds, kupitia kipindi chake cha
‘Njia Panda’ kilichorushwa hewani Juni 15 mwaka huu kati ya saa 8.00
mchana na saa 10.00 jioni kilikuwa na mada iliyohusu safari ya kuzimu
ambapo maudhui yake yalijaa simulizi za kufikirika, za kishirikina na
kichawi.
Aidha
alisema kosa lingine kituo hicho hakikufuata kanuni za
Utangazaji(maudhui) za mwaka 2005 zinazowataka kuwasilisha ratiba ya
vipindi vyao kwa TCRA ili viidhinishwe na vilevile kuvichapisha katika
gazeti kabla ya kurushwa hewani ambapo kipindi cha Njia Panda
hakikuwasilishwa kwa ajili ya kuidhinishwa.
Wakati
huo huo, kituo cha televisheni cha Clouds kilirusha kipindi cha ‘Bibi
Bomba’ Mei 16 na Juni 6 mwaka huu kati ya saa 3.00 na saa 4.00 usiku
ambacho kilikiuka kanuni za Utangazaji (maudhui) za mwaka 2005.
Alisema
kipindi hicho kilidhalilisha mabibi hao walioshiriki pamoja na
wanawake kwa ujumla kutokana na maswali ya aibu waliyokuwa wakiulizwa
na waamuzi wa shindano hilo ambayo ni kinyume na kanuni hizo.
Aidha
alisema kituo hicho kinatozwa faini ya Sh milioni moja na kutakiwa
kuwasilisha TCRA mwongozo wa kuchuja na kusimamia maudhui yasiyofaa
kabla ya kutangazwa.
TCRA imesema kama Kanuni za Utangazaji zitaendelea kukiukwa hatua kali zaidi za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Chapisha Maoni