Unknown Unknown Author
Title:
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
HOME Madhara ya kiikolojia katika matumizi ya maliasili katika maisha ya maskini katika Afrika na kanda Nanine hayaangaliwi vya kutosha ...
HOME
Madhara ya kiikolojia katika matumizi ya maliasili katika maisha ya maskini katika Afrika na kanda Nanine hayaangaliwi vya kutosha na mijadala ya maendeleo, wanasema wataalam wa misaada.

ACCRA, Septemba 5 (IPS) -
"Afrika inajulikana kama moja ya mabara tajiri zaidi duniani linapokuja suala la maliasili, hata hivyo pia ni ukanda fukara zaidi – pamoja na kuwa na utajiri wa asili na kumiminika kwa misaada mingi," alisema Charles Mutasa, mkurugenzi mtendaji wa Jukwaa la Afrika na Mtandao wa Kupambana na Madeni na Maendeleo (AFRODAD) –NGO yenye makao yake makuu mjini Zimbabwe ambayo inafanyia kazi tatizo la madeni la Afrika.

Mutasa alikuwa mshiriki katika mjadala wa Mkutano wa Tatu wa Watu Maarufu juu ya Ufanisi wa Misaada (HLF3), ambao ulifanyika katika mji mkuu wa Ghana wa Accra kuanzia Septemba 2-4.

"Deni la kiikolojia lililosababishwa na matumizi kupita kiasi ya maliasili linachangia kwa kiasi kikubwa katika hali hii," Mutasa aliongeza. "Inalifanya bara kuwa chini, inazuia ukanda kutokujinasua kutoka kwenye mzunguko wa umaskini, na kuchochea haja ya misaada zaidi."

Neno deni la kiikolojia lina maanisha deni lililokusanywa na mataifa tajiri kwenye nchi zinazoendelea kutokana na matumizi ya rasilimali ya kupita kiasi, ambalo mara nyingi linasababisha matatizo ya kimazingira kama vile uchafuzi wa maji na hewa.

"Pande chache mno ambazo ni sehemu ya mjadala wa maendeleo zinaona umuhimu wa kuliangalia deni la kiikolojia na madhara yake katika maisha ya watu," anasema Brenda Mofya, mwanaharakati wa kutoa ushauri nasaha juu ya madeni na mwandishi wa madhara ya kiikolojia yatokanayo na migodi ya shaba nchini Zambia. Ripoti hiyo itazinduliwa mwishoni mwa mwezi Septemba 2008.

Zambia ni taifa la saba duniani kwa kuzalisha shaba. Mwaka 2007 nchi hiyo ilizalisha tani 521,984 za shaba; mwaka huu serikali inategemea uzalishaji kuongezeka hadi tani 600,000.

Hata hivyo, Mofya alisema, serikali ya Zambia na watu wake hawaonekani sana katika utajiri unaotokana na migodi ya shaba ambayo iko chini ya sekta binafsi – ikiwa ni pamoja na makampuni mengi ya kigeni.

"Serikali ya Zambia inapata tu asilimia 0.06 ya faida kwa mwaka. Wakati huo huo makampuni ya madini yanazidi kutajirika, na matatizo ya kiikolojia yanazidi kukusanyika. Mambo haya yana madhara makubwa kwa maisha ya watu," alisema.

Aliiambia IPS kuhusu ubora duni wa hewa katika ukanda wa shaba, ambayo haifikii vigezo vya kimataifa.

"Vumbi la madini na taka vinasababisha matatizo ya kiafya na kimazingira. Tuligundua kuwa kati ya madampo 45 ya taka, 32 yameshajaa. Vumbi hili na taka nyingine vina madhara hasi katika maji pia."

Kulingana na Mutasa, mataifa tajiri yaliyoshiriki katika unyonyaji wa utajiri wa Afrika yanapaswa kukaa mezani na kulipia deni ambalo limejikusanya katika Afrika. "Kama tunataka Afrika kuendelea, tunahitaji kuangalia suala hili kwa umakini mkubwa." 

About Author

Advertisement

Chapisha Maoni

 
Top