HOME
LEO nimelazimika kuendeleza mjadala niliouanzisha wiki iliyopita ukiwa na kichwa ‘Porojo za Membe na umasikini wa Tanzania’.
Ulikuwa ni mjadala unaohusu kauli za Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataif,a Bernard Membe alizozitoa wakati wa kufunga kongamano la uhuru lililofanyika katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam hivi karibuni.
Leo nitaeleza kwa ufupi tu kwa nini Tanzania ni masikini kwa miaka yote 51 ya uhuru na kutoa mapendekezo ya kujikwamua, tofauti na Waziri Membe alisema ni ndoto ya mchana kuzungumzia maendeleo kwa miaka 51 tu.
Tuanze kwa kuangalia historia ya utawala wa nchi yetu tangu wakati wa Mwalimu Nyerere aliyekuwa Waziri mkuu wa kwanza na baadaye rais.
Baada ya kuingia madarakani Mwalimu Nyerere alifanya mabadiliko makubwa ikiwa ni pamoja na mfumo wa utawala kutoka ule wa kifalme (Westminster) na kuunda Jamhuri na yeye akawa Rais. Lengo lilikuwa ni kuwa na mamlaka yote ya kuiongoza nchi.
Aliendelea kufanya mabadiliko kiasi hata cha kuiminya demokrasia hasa pale alipoziua asasi za kiraia na baadaye kufuta mfumo wa vyama vingi mwaka 1965.
Mwaka 1967 Mwalimu Nyerere alianzisha Azimio la Arusha lililosimika sera ya Ujamaa na Kujitegemea. Kupitia azimio hilo Serikali ilitaifisha rasilimali za uchumi na huduma za jamii zilizokuwa mikononi mwa watu binafsi na makampuni.
Pamoja na mambo mengine, Mwalimu Nyerere alipoteza muda mwingi katika ukombozi wa Bara la Afrika miaka ya 1960 na 70 wakati nchi yetu ikiwa kwenye nchi zilizo mstari wa mbele katika mapambano ya kuikomboa Afrika.
Haikuwa vibaya lakini hiyo ni sababu ya kurudi nyuma kiuchumi. Kama hiyo haitoshi, hata ile vita ya Uganda mwaka 1978/ 79 nayo iligharimu maendeleo ya uchumi.
Sababu nyingine iliyokwamisha maendeleo ilikuwa ni maadui wa sera ya ujamaa na kujitegemea. Kulikuwa na maadui wa aina mbili, kwanza ni mataifa ya kibepari na vyombo vya fedha vya kimataifa yaani IMF na WB ambavyo vilipigana kufa na kupona kutia mikono yake kwenye Serikali.
Maadui wengine walikuwa wa ndani, yaani wasaidizi wa Nyerere. Alikuwa amezungukwa na wanafiki ambao walimkubalia tu machoni lakini myoyoni hawakuwa naye kabisa. (Soma kitabu cha Maadili na hatima ya Tanzania: Ibrahim Kaduma).
Ndiyo hao waliokutana Zanzibar mwaka 1991 na kuliua Azimio la Arusha kwa kulegeza masharti yake.
Baada ya Mwalimu Nyerere, viongozi waliofuatia walibadilisha kabisa sera ya ujamaa. Hadi leo Tanzania haijulikani, inafuata itikadi gani, ujamaa na kujitegemea au ubepari?
Ndiyo tukaona zama za mzee ruksa yaani Rais Ali Hassan Mwinyi ambaye alijitahidi kuondoa ukiritimba wa upatikanaji wa bidhaa na huduma za jamii. Japo ruksa zake hizo ziliingiza wema na wabaya serikalini.
Utalawa wa Benjamin Mkapa utakumbukwa kwa kuimarisha ukusanyaji wa kodi na kuimarisha mapato ya Serikali.
Lakini pia utakumbukwa kama utawala uliokithiri kwa kashfa za ufisadi kama vile wizi wa fedha katika Benki Kuu (EPA), viongozi kujimilikisha ardhi za vijiji, huku mwenyewe Mkapa na Waziri wake wakidaiwa kujimilikisha mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira mkoani Mbeya.
Ni katika utawala huo ndipo sera za ubinafsishaji na uwekezaji zilishika kasi. Hapo ndipo kukawa na uwekezaji mkubwa katika sekta ya madini, viwanda na mawasiliano.
Utawala wa sasa wa Rais Jakaya Kikwete umerithi mambo mengi ya Mkapa bila kufanya mabadiliko makubwa.
Jambo kubwa linalojidhihirisha katika tawala hizi tatu ni kukithiri kwa ukosefu wa maadili hasa kwa viongozi wa umma. Viongozi wengi wamejitajirisha kupitia nafasi zao huku idadi kubwa ya Watanzania ikiendelea kuwa masikini.
Pamoja na mikakati mingi ya maendeleo, bado umasikini umeendelea kutawala. Mikakati hiyo inashidikana kutokana na viongozi wa Serikali kutokuwa waaminifu.
Kibaya zaidi hakuna anayekiuka maadili na kuchukuliwa hatua. Hii ndiyo sababu kubwa ya umasikini wa Tanzania.
Suluhisho ni kubadilisha mfumo mzima wa Serikali na kuweka kizazi kitakachochukia rushwa, wizi, uzembe na matumizi mabaya ya madaraka yaliyokithiri Serikalini.
CCM imejaribu mara kadhaa imeshindwa, hata mkakati wa kujivua gamba umeshindikana kabisa. Tunahitaji chama makini kitakachotuvusha hapa tulipo.

Chapisha Maoni