HOME
Chama
cha demokrasia na maendeleo (chadema)jimbo la Geita kilichofakuwa
kikifanya kampeni zake kwa kutumia usafiri wa pikipiki ya miguu
mitatu(bajaji)kimeibuka kidedea katika uchaguzi wa serikali za mitaa
kwenye halmashauri ya mji wa Geita na kukishinda chama cha mapinduzi
(CCM)ambacho kilikuwa kikifanya kampeni zake kwa kutumia usafiri wa
helkopita(CHOPA)ya mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita Joseph Musukuma.
Katika
uchaguzi huo,mbali na kasoro nyingi zilizojitokeza ikiwemo mkurugenzi
wa halmashauri ya mji wa Geita kudaiwa kukibeba Chama Cha
Mapinduzi,halmashauri ya mji wa Geita yenye mitaa 65,Chadema imejizolea
mitaa 33,cuf mtaa 1 na ccm mitaa 18,ambapo katika mitaa hiyo,mitaa 3 ccm
waliipata kwa kuweka pingamizi kwa wagombea na kuondolewa huku mitano
ikishindwa kushiriki kutokana na sababu mbalimbali.
Hata hivyo baadhi ya wananchi katika Halmashauri ya mji Geita wamemtaka Waziri wa tawala za mikoa na Serikali za mitaa
Hawa Ghasia kumchukulia hatua kali mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa
Geita Magreth Nakainga kwa kuvuruga na kuchakachua matokeo ya uchaguzi
wa mitaa katika mji wa Geita.
Mkurugenzi
huyo anatuhumiwa kuingilia baadhi ya vituo vya kupigia kura na kufuta
matokeo na kutangaza uchaguzi urudiwe baada ya kugundua wagombea wa CCM
wameshindwa katika matokeo hayo.
Hata
hivyo mbali na uchakachuaji huo,mji wa Geita wenye mitaa 65,Chadema
imejizolea mitaa 33,cuf mtaa 1 na ccm mitaa 18,ambapo katika mitaa
hiyo,mitaa 3 ccm waliipata kwa kuweka pingamizi kwa wagombea na
kuondolewa huku mitano ikishindwa kushiriki kutokana na sababu
mbalimbali.
Mitaa ambayo mkurugenzi huyo alitangaza matokeo kinyume na kanuni za uchaguzi ni pamoja na mtaa wa Elimu, Mission na Katoma.
Matokeo
ya mtaa wa Katoma yalikuwa ni mgombea wa chama cha demokrasia na
maendeleo (chadema) alishinda kwa kura 428 tofauti kubwa ya kura dhidi
ya mgombea wa chama cha mapinduzi (ccm) aliyepata kura 364.
Mgombea
wa chama cha demokrasia na maendeleo (chadema) ni Patrick Faida na
mgombea wa chama cha mapinduzi (ccm) ni Aloyce Bayona
Aidha
mtaa mwingine ambao inadaiwa mkurugenzi huyo alitangaza matokeo kwa
kutumia jeshi la polisi ni mtaa Elimu kata ya Nyankumbu mjini Geita
ambapo wapiga kura walikuwa wameisha vamia kituo cha kupigia kura na
kuvunja masanduku ya kura,kuchana karatasiza kura na msimamizi msaidizi
kukimbia.
Baada
ya mkurugenzi kupata taarifa ya kituo kuvamiwa na wapiga kura kwa madai
kwa msimamizi msaidizi kudai kura zimezidi idadi ya waliopiga
kura,mkurugenzi alifika akiwa na polisi wapatao wane na kutangaza kuwa
mgombea wa chama cha mapinduzi ameshinda.
Katibu
wa chadema Jimbo la Geita,Mutta Robert,alisema kuwa kulikuwa na njama
za kuhakikasha mitaa yote ya Halmashauri ya mji wa Geita inatangazwa
matokeo yake kwa ubabe kwa kutumia jeshi la Polisi ili kuisaidia ccm.
“Tulipata
taarifa mapema kwamba mkurunzi wa mji wa Geita kwa kushirikiana na CCM
wamepanga kutumia polisi kutangaza matokeo ya mitaa kwa nguvu baada ya
kubaini kuwa chadema itashinda mitaa mingi”,aliiambia Malunde1 blog
“Tuliimarisha
ulinzi kwa kutumia brigedia nyekundu ya ulinzi ya chama chetu na
kuwaelewa wapiga kura wetu mapema njama za ccm za kutaka kuiba kura kwa
kutumia polisi,wapiga kura waliakikisha wamepiga na kulinda kura zao.”
Alisema
kuwa baadhi ya vituo ambavyo wapiga kura walijisahau kidogo mkurugenzi
huyo alitumia nafasi hiyo kutangaza mgombea wa chama cha mapinduzi.
Robert
alisema kuwa mtaa wa Mission na mtaa wa Elimu idadi ya kura zilizokuwa
kwenye sanduku la kura zilizidi idadi ya watu waliojitokeza kupiga kura
na mkurugenzi huyo alitangaza matokeo na kuwapa ushindi wagombea wa
chama cha mapinduzi,lakini mtaa wa Katoma ambao idadi ya kura ilizidi
wapiga kura na mgombea wa chadema kushinda,mkurugenzi huyo alifuta
matokeo.
“Huyu
mkurugenzi alikula njama mapema, maana mitaa yote 60 ya Halmashauri ya
mji wa Geita ilikuwa na karatasi pungufu na sehemu
nyingine nilipompigia simu kumweleza mapungufu hayo alipeleka karatasi
za kura baada mawili kupita na alipokuwa akipeleka zingine zilikuwa
zinakuwa za kituo tofauti na hicho” alisema Robert.
Mkurugenzi
alisema kuwa hayo ni matatizo madogo madogo yaliyotokea nchi nzima na
sio kwenye Halmashauri yake tu na hakutegemea kama wapiga kura
watakuwa wengi ndiyo maana alikuwa anapeleka karatasi chache chache
vituoni.
Kuhusu madai ya Katibu wa chadema Mutta Robert kuwa mkurugenzi alikuwa na njama na ccm na kutangaza matokeo kibabe alisema ,
“Hivi huyu kijana kwa chadema ni nani? Ni msumbufu sana lakini inaonekana anajaza mambo yasiyo ya kweli”.
Mji
wa Geita una mitaa 65 lakini iliyoshiriki uchaguzi huu ni 60 na kati ya
hiyo,Chadema imejizolea mitaa 33,cuf mtaa 1 na ccm mitaa 18 lakini
mitaa 3 ccm waliipata kwa kuweka pingamizi kwa wagombea na kuondolewa.
Hivyo
kwenye matokeo ya kupigiwa kura,ccm imepata mitaa16 tu na mitaa 4
uchaguzi wake unafanyika jumapili wiki hii ambapo chadema inaonekana
kuwa na ushawishi mkubwa katika mitaa hiyo.Mitaa hiyo ni Katoma,Nyerere
road,Mwatulole na Lwenge.
Malalamiko
haya yanakuja siku moja baada ya waziri wa tawala za mikoa na serikali
za mitaa Hawa Ghasia kutangaza kuwa mtumishi wa serikali yeyote
aliyeshiriki kuharibu uchaguzi huu atashughulikiwa na kuwajibishwa mara
moja na tayari wengine wameshaanza kuwajibishwa .
Na Victor Bariety-Malunde1 blog Geita
Chapisha Maoni