HOME
Waziri Hawa Ghasia ameanza kuitekeleza ahadi yake, Wakurugenzi hawa wamesimamishwa kazi
Siku chache baada ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu
TAMISEMI Hawa Ghasia kuahidi kumuwajibisha yoyote aliyehusika na
kuvuruga uchaguzi wa Serikali za mitaa uliofanyika tarehe 14, leo Waziri
huyo ametangaza majina ya Wakurugenzi watano waliosimamishwa kazi na
wengine sita waliopewa onyo kutokana na uchunguzi kuonyesha wameshindwa
kutekeleza wajibu wao.
Majina ya Wakurugenzi waliotajwa kusimamishwa ni haya; Felix Mabula (Halmashauri ya Hanang), Fortunatus Fwema (Halmashauri ya Mbulu), Isabella Chilumba (Halmashauri ya Ulanga), Pendo Malabeja (Halmashauri ya Kwimba) na William Shimwela (Halmashauri yaSumbawanga).
“…Ni
dhahiri kuwa Wakurugenzi wa kwenye zile Halmashauri zenye dosari
wameonyesha udhaifu mkubwa sana wa kutekeleza majukumu yao ikiwemo
jukumu la msingi la kusimamia uchaguzi ambao ni moja ya majukumu ya
Wakurugenzi. Kasoro hizo zilisababisha kurudiwa kwa uchaguzi katika
baadhi ya maeneo yao… Wakurugenzi hao wametenda makosa yafuatayo ambayo
yanawaondolea sifa ya kuwa wakurugenzi katika halmashauri…“– Hawa Ghasia.
“…
Kwanza ni kuchelewa kuandaa vifaa vya kupigia kura, kukosa umakini
katika kuandaa vifaa vya kupigia kura na hivyo kuchanganya majina pamoja
na vyama, kuchelewa kupeleka vifaa kwenye maeneo ya kupigia kura,
uzembe katika kutekeleza majukumu yao na kutoa taarifa za kupotosha
kuhusu maandalizi ya uchaguzi.. kwa sababu walituhakikishia kwamba
maandalizi yamekamilika huku wakifahamu kwamba suala hilo sio kweli…“– Hawa Ghasia.
Hapa unaweza kumsikiliza Waziri huyo wakawi akizungumzia taarifa hiyo.
https://www.hulkshare.com/playlist/122712
Chapisha Maoni