HOME
KUHUSU MAPACHA KUTOKA TANZANIA WALIOKUWA WAMEUNGANIKA CHINI YA KIFUA NA TUMBONI
Hospitali ya Apollo iliyoko nchini India imefanikiwa
kuwatenganisha mapacha wa kike wa Tanzania Abriana na Adriana waliokuwa wameunganika chini ya kifua na tumboni katika upasuaji uliofanyika tarehe 17 Novemba 2014 nchini humo.
kuwatenganisha mapacha wa kike wa Tanzania Abriana na Adriana waliokuwa wameunganika chini ya kifua na tumboni katika upasuaji uliofanyika tarehe 17 Novemba 2014 nchini humo.
Mapacha
waliounganika kwa mtindo huu hujulikana kwa watalaam kama Thoraco
Omphalopahus na upasuaji uliofanyika na hospitali Apollo ulikuwa wenye
mafanikio na wa aina yake.
Mapacha Abriana
na Adriana awali ya upasuaji huo walikuwa wameunganika kuanzia chini ya
kifua na tumbo, hali kadhalika walikuwa wakitumia mvungu mmoja wa moyo
na maini yaliyounganika.
Changamoto
ya upasuaji wa mapacha hawa kwa madaktari ulikuwa utenganishaji bila
kuwavujisha damu nyingi ambayo waliweza kukabiliana nayo ipasavyo.
Upasuaji
huo ulifanywa na jopo la watalaamu 50 waliobobea katika taaluma mbali
mbali za tiba ya afya ya kabla na baada ya upasuaji ambao uliendelea kwa
masaa 11.
Watalaamu
walifanikiwa kutenganisha viungo vilivyokuwa vimeungana. Mapacha hawa
walipona na kupata ahueni kwa haraka hivo kusaidia zoezi zima la
uponyaji baada ya upasuaji.
Hali
kadhalika, hatua nyingine ya muhimu katika upasuaji huo ilikuwa
kurudisha viungo husika mahala pake baada ya kuvitenganisha.
Akizungumzia
kuhusu hili Dkt. K S Sivakumar Plastic & Reconstructive
Surgeon anasema, “Baada ya upasuaji, moyo wa moja ya mapacha ulitakiwa
kurudishiwa mahali pake ili kuzuia mbenuko na uharibifu pamoja na maini
yaliyokuwa yameungana
. Ilichukua majopo mawili ya wataalum kwa masaa nne kukamilisha ufungaji wa maini, moyo, na utumbo katika mahala pake.”
VIA:MALUNDE1 BLOG
Chapisha Maoni