HOME Kenyatta asaini sheria kali ya usalama Rais ...
HOME
Kenyatta asaini sheria kali ya usalama
Rais Uhuru Kenyatta
Rais
wa Kenya Uhuru Kenyatta, ameidhinisha sheria mpya ya usalama ambayo
inawezesha majasusi kunasa mawasiliano kisiri au kufanya udukuzi pamoja
na kuwazuia washukiwa wa ugaidi kwa mwaka mmoja kabla ya kuwafungulia
mashitaka.
Kenyatta anasema kuwa sheria hiyo mpya inahitajika kwa
ajili ya kukabiliana na tisho la ugaidi kutoka kwa kundi la wapiganaji
wa kiisilamu la Al Shabaab.
Amesisitiza kuwa sheria hio haikiuki haki za binadamu wala kuwapokonya watu uhuru wa kujieleza.
Mnamo
siku ya Alhamisi, wabunge wa serikali na wa upinzani walipigana makonde
bungeni wakijadili marekebisho kwa mswada kabla ya Rais kuupitisha kuwa
sheria.
Katika vurugu hizo mmoja wa wabunge wa upinzani alimmwagia maji naibu spika.
The part time Blogger love to blog on various categories like Web Development, SEO Guide, Tips and Tricks, Android Stuff, etc including Linux Hacking Tricks and tips. A Blogger Template Designer; designed many popular themes.
Chapisha Maoni