HOME
Maamuzi ya Rais Kikwete kuhusu maazimio ya Bunge, kuwawajibisha Mawaziri na akaunti ya Tegeta Escrow
Rais Kikwete
leo December 22 amehutubia Taifa kwa kufanya mazungumzo na wazee wa Dar
es Salaam ambapo amezungumzia mambo makuu mawili; kwanza kuhusu
Uchaguzi Serikali za Mitaa na pia maazimio ya Bunge kuhusu uchotwaji wa
pesa kwenye akaunti ya Tegeta Escrow.
Kuhusiana na maamuzi yaliyotolewa na Waziri Hawa Ghasia kwa Wakurugenzi ambao hawakuwajibika kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Rais Kikwete amesema; “Katika
taarifa ya waziri Ghasia alielezea kasoro zilizojitokeza na aliahidi
kuchukua hatua. Nieleze furaha yangu kwa Hawa Ghasia juu ya hatua
alizochukua na mimi nikaweka ridhaa yangu…“
Rais Kikwete alitolea ufafanuzi wa uhalali wa fedha za Escrow kuwa mali ya umma ama mali ya IPTL; “…Maelezo
haya kwa kiasi fulani yanasaidia kwenye kupata jibu la swali maarufu,
fedha hizi hasa mwenyewe nani? Akaunti ya Escrow ni akaunti maalum
inayoanzishwa kwa ajili ya sababu maalum, kufanya kazi maalum, kwa
masharti maalum na kazi hiyo ikiisha na akaunti yenyewe inafungwa…
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali akasema aaah.. nyinyi si
mliletewa madai? Si mmelipa? Hata kama hazijaenda kwa mwenyewe
msizihesabu kuwa ni zenu, hizi sio zenu…”
“Fedha
zilizowekwa kwenye akaunti ya Escrow hazina sifa ya kutafsiriwa kama
ni mali ya TANESCo, hivyo marekebisho yamefanywa ili kutotambua mali na
madeni yanayohusu fedha hizo kwa kiasi cha fedha zilizopo kwenye akaunti
ya Escrow… Ni dhahiri kwamba fedha zilizokuwa kwenye akaunti ya Escrow
sio za TANESCo na hazikupaswa kuingizwa kwenye vitabu vya TANESCo kama
mali yake… Kama si za TANESCo ni za IPTL…“
Bodi
ya TANESCo iliyopo sasa imemaliza muda wake tumeanza mchakato wa Bodi
mpya… Katibu Mkuu wa Wizara tumejadili hili katika Serikali tukasema
huyu ni Mtumishi wa Umma.. nimeagiza mamlaka zinazohusika na mchakato
huu wazichunguze tuhuma zinazohusika ili kama itadhihiri basi
awajibishwe inavyostahiki…“
“...
Mwanasheria Mkuu wa Serikali ameshajiuzulu… Waziri wa Ardhi kupokea
fedha kutoka VIP Engineering & Marketing, mazungumzo yetu sana
yalikuwa pesa hizi ni za nini, amezipata vipi, kwa ajili gani? Ameeleza
kuwa pesa ni za shule… maswali makubwa ambayo yametia shaka sana
nakuleta mjadala mkubwa ni kwanini pesa hizi hazikwenda moja kwa moja
kwenye shule zikawa kwa jina lake… Tulikubaliana kwamba Waziri huyu na
tulikwishazungumza naye kwamba atupe nafasi tumteue mwingine…“– Rais Kikwete.
Unaweza kuzisikiliza taarifa hizo kwa kubonyeza play hapa.
http://www.hulkshare.com/millard_ayo_/jk-bodi-ya-tanesco-katibu-mkuu-wizara-ya-nishati-waziri-tibaijuka
http://www.hulkshare.com/millard_ayo_/jk-bodi-ya-tanesco-katibu-mkuu-wizara-ya-nishati-waziri-tibaijuka
http://www.hulkshare.com/millard_ayo_/jk-hawa-ghasia
http://www.hulkshare.com/millard_ayo_/jk-bodi-ya-tanesco-katibu-mkuu-wizara-ya-nishati-waziri-tibaijuka
http://www.hulkshare.com/millard_ayo_/jk-bodi-ya-tanesco-katibu-mkuu-wizara-ya-nishati-waziri-tibaijuka
http://www.hulkshare.com/millard_ayo_/jk-hawa-ghasia
Chapisha Maoni