,huu ndi mchanganuo wa aliyoyasema raisikkikwete kuhusu ESCROW hii leo.
iii). PESA ZILIKAA KWENYE ACCOUNT YA ESCROW KWA MIAKA 7.
iv) .Wakati CAG anakagua kulikuwa na shilingi 202 Bilioni nukta tisa.
v) Kama Tanesco wangeli tozo za uwekezaji,akaunti hii ingekuwa na
shilingi Bilini 306.7,kutokana na Tanesco kutolipa ilibaki na madeniya
shilingi Dola Bilioni 33.6 na IPTL.
vi) .Account ya Ecsrow haikuwa na Bilioni 306,bali zilikuwemo Bil 202 pekee ambazo IPTL ilikuwa inaidai Tanesco.
vii).Amesema kuwa kutoka na hali ya mgogoro ulivyokuwa pesa zilizokuwa
ndani ya akaunti ya ESCROW SI ZA UMMA BALI NI ZA IPTL kwani ndiyo
mlipwaji kutokana na madeni ambayo IPTL inaidai TANESCO kutokana na tozo
za uwekezaji.
vii).Kuhusu majibu ya CAG,kuhusu pesa ni za nani?raisi amesema kama
Tanesco wangeshinda mgogoro wao na IPTL basi pesa hizo zingekuwa za UMMA
kama ilivyokuwa kwenye kesi yao ya mwaka 2001,ila kwa sababu Tanesco
walishindwa,pesa hizi ni za IPTL na si UMMA(PUBLIC)
viii),KUHUSU KUWEMO KWA KODI ZA SERIKALI NDANI YA ESCROW ACCOUNT KIASI
CHA BILIONI 21 NA MILIONI 700,AMESEMA PAP WALIPELEKEWA DENI LA KODI YA
SERIKALI,AMESEMA CAG ALIKAGUA NA KUSEMA PESA ZILIZOKUWEMO KWENYE AKAUNTI
YA ESCROW HAZIKUWA NA SIFA ZA KUITWA PESA ZA UMMA.
ix).Trh 15.9.2013 mahakama kuu ya Tanzania ulifanya uamuzi wa maombi ya
kampuni ya VIP kuomba kusimamisha mchakato wa kuuza hiza za IPTL
wakilumbana juu ya hisa,uamuzi wa mahakama ulikuwa PAP wapewe hisa 30 NA
WAKANUNUA HISA 70 na waliandikisha hisa 70 Brela,mahakama ikaamua hisa
zikabidhiwe PAP ambao ndiyo mmiliki halali wa IPTL.,Uamuzi huu wa
mahakama ulimaanisha kuwa PAP wanatakiwa kumiliki mpaka pesa za ESCROW
kwa PAP,umauzi ambao ulizuia malumbano serikalini juu ya akauniti
ifungwe ama isifunwe,pesa zitoke ama zisitoke.
x).Wizara ya nishati na madini waliamu kuomba ushauri kwa mwanasheria
mkuu juu ya pesa,AG alielekeza kuwa pesa zilipwe kama mahakama
ilivyotaka,benki kuu waliuliza maswali haya,na AG akaelekeza walipe kwa
PAP na hakuna kodi,ushsuri wa AG uliitoa nafasi ya akaunti kufungwa na
kugawanywa rasmi na baadae kuingia barabarani.
xi).Maamuzi yote yaliyofanyika yalifanyika kwa maelekezo ya mwanasheria
mkuu,umuzi huu wa mwansheria kuu umeibua mjadala mkuu kuwa kuna rushwa
kubwa,watu wamemegewa mshiko,kila mtu kaongea.
xii).Amekanusha kuwa kufungwa kwa akaunti ya ESCROW hakukuwa na msukumo
kutoka kwa maafisa wa serikali,amesema serikali ilifanya juhudi kubwa
kwenye sakata hili.
xii).Amesema mwanasheria mkuu alimwambia hakukuwa na makosa yeyote
kwenye maamuzi ya mahakama,na pia hakuna hasara ambayo serikali imepata
kutokana na sakata hili la ECSROW kwa sababu pesa hizo zilikuwa ni deni
ambalo Tanesco ilikuwa inadaiwa na IPTL.
xiii).Kuhusu kuwa PAP walinunua hisa za PIPAL LINK huku kikuwa na amri
ya mahakama ya kutouza hisa,amesema bado vyombo vya mamlaka vinachunguza
xiv).Kuhusu uuzwaji wa hisa,amesema napo kunahitaji uchunguzi zaidi hasa bei ya hizi hisa.
xv).Amesema Rugemalira alilipa kodi aliyokuwa anadaiwa kiasi cha
shilingi Bilioni 38,RUGEMALIRA hana makosa kwenye hili,Alilipa kodi
zote.
xvi).KUHUSU MAPENDEKEZO CAG ameelekeza taaifa zile zipelekwe PCCB.
xvii).Kuhusu waliomegemewa pesa na RUGEMALIRA,amesema Takukuru na tume
ya maadili ya watumishi wa umma wanachunguza na kushuhulika na watumishi
wa umma wote waliopewa pesa,amesema tume ya maadili ya umma itawahoji
wote waliopewa pesa.
KUHUSU MAZIMIO YA BUNGE
i.Amesema serikali imeyapokea maazimio na itayafanyia kazi
ii.Kuhusu kutaifisha mitambo ya IPTL,amesema si sawa kutaifisha sababu kutafukuza wawekezaji
iii.Kuhusu uwazi wa mikataba,amesema serikali itafanya mapitio ya
mikataba,amesema kuna haja ya serikali na bunge kukaa pamoja na
kuzungumza,kwa sababu kuna makampuni yanataka usiri wa mikataba(company
secret)
iv)Kuhusu PCCB,na vyombo vingine vya ulinzi na usalama vichukue hatua,amesema tayari utekelezaji ueanza.
v).Kuhusu kuwavua vyeo wenyevitio wa kamati amesema bunge ndilo litekeleza.
vi).Kuhusu kuundwa kwa tume ya kijaji kuwachunguza majaji waliohusika na
sakata la ESCROW,amesema itabidi kuzingatia utaratibu wa kikatiba na
sheria,amese suala hili linatakiwa kuanzia kwenye mahakama,halianzii kwa
raisi wala bungeni,Amemuachia Jaji mkuu alishughulikie na kumpelekea
mapendekezo raisi.
vii).Kuhusu mamlaka husika za kifedha na kiuchunguzi ziitaje Stanbic
bank na benk zilizohusika zitangazwe kuwa taasisi zinazotakatisha fedha
amesema uchunguzwe na mamlaka husika.
viii).Kuhusu serikali iandae na kuwasilisha marekebisho ya sheria ya
uundwaji wa rushwa kubwa,amesema hilo ni wazo zuri,na serikaliimekuwa
inaifanyia marekebisho taasisi ya kuzuia rushwa tangia mwaka 2008
ix).Kuhusu kuwavua nafasi zao watumishi wa umma wakiwemo mawaziri
waliotajwa,raisi Kikwete amesema,Bodi ya Tanesco imeshamaliza muda
wake,hili lishajifuta,kuhusu katibu mkuu Maswi amesema mamlaka
zinazohusika zianze ushunguzi wa kuchunguza tuhuma zake,mwanasheria mkuu
ameshajiuzulu,kuhusu mawaziri(TIBAIJUKA) amesema wamezungumza nae na
wamekubaliana aachie ngazi,kuhusu Prof Muhongo amemuweka kiporo..
NAJIPA MUDA KABLA SIJATIA NENO.