HOME
Sio Movie… Watoto wavamia Bank… Tazama video ya kilichotokea hapa
Movie zimelalamikiwa kuharibu watoto mara nyingi, wanachokiona wao hukibeba na kukipelleka kwenye uhalisia kwa kuwa wanakuwa hawana utashi wa kutambua kwamba wanachokiona kwenye movie sio kitu halisia, bali ni maigizo.
Watoto wawili wenye umri wa miaka 12 na mwingine 13, wamepandishwa kizimbani wakituhumiwa kufanya jaribio la kuiba Bankwakitumia Bastola bandia.
Haikuwa movie, hii ni kweli kutoka Israel.
Mmoja wao alikuwa amebeba begi la daftari mgongoni, huku wakiwa na bastola za toy halafu wakaingia benki na kuwatisha wateja waliokuwemo ndani ya Benki hiyo mitaa ya Tel Aviv.
Msemaji wa Polisi huko Israel Micky Rosenfeld amethibitisha tukio hilo kuytokea na kusema kuwa waliwakamata watoto hao baada ya kupata picha za kwenye camera za CCTV.
Mwanasheria Gil Gabay amekosoa namna ambavyo watoto hao walihudumiwa wakiwa kituo cha Polisi, waliwekwa kama watuhumiwa watu wazima huku wakiwafuatilia kwenye camera maalum huku wakiwa wamekaa kwenye viti ambapo Gabay amesema haki za Watoto hao zimekiukwa.
Tayari wamefikishwa Mahakamani na kusomewa mashtaka huku wakiwa wameficha sura zao.
Tumia Sekunde 46 kutazama Video ya tukio hilo la aina yake.
Chapisha Maoni