HOME
Sentensi tano za Rais Museveni kuhusu msimamo wake na Mahakama ya ICC…
Jana December 12 ilikuwa ni siku ambayo Kenya walikuwa wakisherekea maadhimisho ya siku ya Uhuru wa nchi hiyo, viongozi kadhaa wa Afrika walikuwepo Nyayo Stadium kushiriki na Wakenya kwenye maadhimisho ya siku hiyo.
Kulikuwa na maongezi yakiendelea ambapo viongozi mbalimbali wa Afrika hawakupendezwa na kitendo cha Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta kufunguliwa mashtaka kwenye Mahakama ya ICC huku mjadala wa viongozi hao ikiwa ni kujitoa kwenye Mahakama hiyo.
Kama ulipitwa na story hiyo, hapa kuna kile kilichozungumzwa na Rais wa Uganda, Yoweri Museveni kuhusu msimamo wake na Mahakama ya ICC.
“… Nitaleta motion kwa African Union kikao kijacho.. Nataka sisi wote tutoke kwenye Court hiyo ya wazungu wakae na Court yao… Hiyo Court niliunga mkono mwanzoni kwa sababu mimi ni mtu ambaye napenda nidhamu, sitaki watu kufanya madhambi bila kuwajibika.. Lakini wameifanya chombo cha kukandamiza Afrika jela kwa hiyo nimemalizana na hiyo court… Sitafanya kazi nao tena…”– Rais Museveni.
Chapisha Maoni