Wanajukwaa kama ilivyo ada kwa maccm kushinda uchaguzi kwa njia haramu, jana usiku Mbunge aliechakachua ubunge halali wa marehemu Shelembi wa chadema, Stephen Masele jimbo la shinyanga mjini, alikamatwa akigawa rushwa.

Makamanda wa CHADEMA ,RB walikuwa wakifuatilia nyendo zake pasipo yeye kujua na ndipo alipoanza kugawa rushwa alikamatwa, na aliapoanza kupewa kichapo, polisi walimuokoa kwa kupiga risasi za moto na mabomu ya machozi.

Taarifa za uhakika zinaeleza alidondosha nyaraka mbali mbali ktk eneo la tukio.
Quote By Combative View Post
Wana Jamvi habari za uhakika nilizozipata ni kuwa Kimeo Stephen Masele amepokea kichapo cha mbwa mwitu jana usiku majira ya saa nne usiku huko Shinyanga maeneo ya Majengo karibia na msikiti alipokuwa ameenda kupiga kampeni ili wenyeviti anaowataka wapite kwa manufaa yake ya baadae hapo mwakani.

Hata hivyo polisi waliwahi eneo la tukio wakamwokoa na akatupiwa ndani ya defender kama mzigo katika purukushani za kumwokoa na alisikika akiwaambia polisi " nashukuru sana kwa kuniokoa" CHEZEA NGUVU YA UMMA WEWE!