HOME
Haya ni majibu ya Mwigulu Nchemba kuhusu ishu ya Escrow, rushwa na kugombea Urais 2015
Siku ya jana January 12 Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha alikuwa katika mahojiano kwenye kipindi cha Dakika 45 cha ITV,
hapa kuna kile alichokizungumza kuhusu ishu ya nini kifanywe kuwabana
wakwepa kodi na wala rushwa, msimamo wake kugombea Urais 2015 na ishu ya
wahusika waliochukua Fedha za Escrow.
“Kwa
nchi yetu, upande mmoja wa hili la kukwepa kodi na upande wa rushwa
ukitaka kukomesha na lenyewe linasubiria Katiba Mpya tutakapokwenda
kwenye Sheria hili tutasimamia mpaka koo litakauka… Yaani mtu kupokea
rushwa anatakiwa anatakiwa akikadiria hivi siku nikipokea rushwa
nikikamatwa madhara yake ni nini…“– Mwigulu Nchemba.
Anatakiwa
ajue siku ileile kwamba hakuna dhamana, taratibu za kimahakama
zitaendelea akiwa ndani nakutoka hapo adhabu yake inatakiwa imtishe…
Kama mtu amesababisha hasara ya bilioni thelathini, kama adhabu nii
kumuondoa tu kwenye nafasi aliyokuwa nayo umempa likizo akatumie fedha…
Umempa send-off akasherekee fedha ya umma…”– Mwigulu Nchemba.
Kuhusu hatua ambazo zimefikiwa mpaka sasa kwa wale waliochukua pesa za Escrow, Naibu Waziri huyo alisema; “Taarifa
nilizonazo tayari Mamlaka ya Mapato imeshafanya hesabu… Kuhusu haya
mambo ya Kodi kweli tumedhamiria, kwamba lazima kodi ilipwe na hili si
jambo la mjadala… Hatuwezi tukasamehe kodi kubwa vile halafu
tukakimbizana na mama anayeuza mchicha…”– Mwigulu Nchemba.
Alipoulizwa kuhusu msimamo wake kwenye Uchaguzi 2015 alijibu; “Ninataka
nifocus sana kumsaidia Waziri kwenye haya majukumu ambayo tumepewa na
Mheshimiwa Rais kuhakikisha kwamba Serikali inatimiza wajibu wake…
Nikirudi kwenye Chama namsaidia Katibu Mkuu kusimamia misingi ya Chama…
Nisingependa niwe miongoni mwa wanaovunja miiko.. Tutavuka mto
tukishafika mtoni kufuatana na taratibu zetu…”– Mwigulu Nchemba.
Msimamo wangu kwenye masuala ya msingi yanayohusu taifa letu huwa hauyumbi wanaonifahamu wanajua…”
Chapisha Maoni