HOME
Nimekuletea taarifa hii ya matumaini kwa watu wa Mali kuhusu Ugonjwa wa Ebola
Mwaka
2014 haukuwa mwaka wenye story nzuri kutoka nchi za Afrika Magharibi
kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola watu zaidi ya elfu kumi
walifariki na wengine zaidi ya elfu tano wakiripotiwa kuugua ugonjwa
huo.
Umoja ya Mataifa na Serikali ya Mali wametangaza kuwa nchi hiyo haina tena ugonjwa hatari wa Ebola baada ya kutoripotiwa taarifa za mgonjwa yeyote wa Ebola kwa muda wa siku kipindi cha siku 42 zilizopita.
Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kupambana na Ebola ulioandikwa katika ukurasa wa Twitter unawashukuru wafanyakazi wa Afya waliojitolea kupambana na Ebola nchini Mali kwa kuhakikisha ugonjwa huo umedhibitiwa.
Mbali na Mali kuonekana kuathiriwa na
ugonjwa huo, Guinea, Sierra leone na Liberia ni mataifa ambayo yamepata
athari kubwa kutokana na ugonjwa huo.
Waziri wa Afya wa Mali amewasifu wahudumu wa Afya na washirika wa Kimataifa kwa msaada wao.
Nimekurekodia taarifa hiyo kwenye kituo cha WBS unaweza kuisikiliza hapa.
Chapisha Maoni